Kenya inasifu mchango wa Misri katika kuimarisha Amani na Usalama barani Afrika.


Monica Juma, Waziri wa  mambo ya Nje wa Kenya  ameusifu mchango wa Misri wakati wa urais wake kwa Umoja wa kiafrika katika kuimarisha masuala ya Amani na Usalama barani Afrika, na hasa  kufanyika  mkutano wa mashauriano ya washirika wa kikanda wa Sudan mjini Cairo hivi karibuni na Rais Abd Elfatah Elsisi, ambao ulihudhuriwa na Waziri anayewakilisha Rais wa Kenya, "Uhuru Kenyatta" .

Wakati wa mkutano, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya alishukuru sana Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri kwa kuendeleza taratibu  pamoja na Kenya kwa maswala mbalimbali yenye umuhimu wa pamoja. 


Hii ilitokea wakati wa mkutano na Balozi Hamdi Sanad Loza, Naibu Waziri wa Mambo ya  nje ya kiafrika na Waziri wa mambo ya nje wa Kenya, Ambapo aliwasilisha ujumbe kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje Sameh Shukri kwake , ambao ulijumuisha njia za kuendeleza mahusiano ya nchi mbili na maswala ya kikanda yenye umuhimu wa  pamoja. 

Mkutano huo pia ulijadili maendeleo ya hivi karibuni kwenye eneo la Pembe ya kiafrika, na kukubaliana juu ya umuhimu wa kuamua wakati wa mkutano wa kamati ya pamoja kati ya nchi mbili  karibuni, ambayo itasaidia kuimarisha ushirikiano kati ya Misri na Kenya.


Ziara ya Naibu wa Waziri wa Mambo ya Nje nchini Kenya ni sehemu ya ziara inayojumuisha Somalia na kanda ya ardhi ya Somalia, kwa kuzingatia ujasiri wa Misri kufuatilia hali ya Afrika Mashariki na Pembe ya kiafrika,sawa ni kwa upande wa kikanda au kwa nchi mbili.

Comments