Mfumo wa kuiga Umoja wa Afrika uko katika masomo ya juu ya Kiafrika huko Kairo
 Jumuiya ya Mawasiliano ya Kiafrika ya Kitivo cha Masomo ya Juu cha Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Kairo ilitangaza kuzindua mfumo wa kuiga Umoja wa Afrika katika toleo lake la kumi na tatu,kutekleza maagizo ya Rais Abd ElFatah El-Sisi, kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano wa pamoja wa Afrika kupitia taasisi za serikali na kuandaa uwezo wa vijana.

 Dokta Rasha Abu Shakra, msimamizi mkuu wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Afrika, alisema kuwa hii inakuja chini ya Uangalifu wa Dokta Mustafa Madbuly " Waziri mkuu", na Dokta Muhamed Othman El Khosht " Mkuu wa chuo kikuu cha Kairo" na kwa uenyekiti wa Dokta Muhamed Nofel " Mkuu wa Kitivo" , Wizara za Vijana na Michezo, Mambo ya nje, Utamaduni, na Kameshina ya Umoja wa Afrika huko Adis Ababa,  wakati wa kuhangaika kwa taasisi zote za serikali zinalenga kuimarisha  ushirikiano wa pamoja wa Afrika kama moja ya alama muhimu zaidi za sera ya nje ya Misri, akiashiria kuwa suala la vijana linatanguliza vipaumbele vya urais wa Jamhuri, na hii ilionyeshwa wazi wakati wa mapendekezo ya Mkutano wa Vijana  wa Dunia 2018 na pia mapendekezo ya Mkutano wa Vijana wa Dunia 2019 .

  "Abu Shakra" ameongeza kuwa programu hiyo inafanyika kwa wiki mfululizo, ndani ya Kitivo cha Mafunzo ya Juu cha Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Kairo, na inalenga vijana 150 wenye utaifa tofauti, na inakusudia kuunga mkono dhana ya umoja wa Afrika, na kupanua madaraja ya mawasiliano kati ya waafrika wamisri na wasio wa wamisri kupitia mawasiliano ya moja kwa moja ili kurekebisha mawazo yenye makosa Kati ya pande hizo mbili, pamoja na kuandaa makada wa Kiafrika na viongozi wenye ujuzi halisi wa kufanya maamuzi katika Umoja wa Afrika, kupanga mkakati wenye lengo la kubadilisha taswira ya akili ya bara la Afrika, kutoa mafunzo na kuwawezesha wanafunzi kwa ujuzi wa mazungumzo na kuamua kupitia semina hizo  zinazoshughulikia masuala ya kweli yanayozikabili taasisi za Umoja wa Afrika kama vile Baraza la Amani na Usalama la kiafrika na mashirika ya Ukamilifu wa kikanda wa kiafrika.

Comments