Wizara ya vijana na michezo yazindua kampeni ya kitaifa kwa kucheza michezo "online"

Dokta Ashraf Sobhy waziri wa vijana na michezo alikubali kuzindua kampeni ya kitaifa ya kiserekali kwa ushiriki wa sekta binafsi kwa lengo la kutosheleza badala za kucheza michezo ili kufanyika  nyumbani kupitia tovuti ya lango la Misri kwa vijana na michezo Emys.gov.eg,  kwa ajili ya kuepuka usambazaji wa virusi ya Corona miongoni mwa hatua za kijikinga na kujiepusha yanayofanywa kwa nchi katika jambo hili . 


Dokta  Ashraf Sobhy alisema kwamba wizara hiyo inafanya kwa mujibu wa njia ya kuhakikisha malengo ya michezo katika nyumba , kama sehemu ya jukumu la huduma na jamii inayofanyiwa na wizara ya vijana na michezo kati ya shughuli za kujikinga na kuepuka ili kupambana na virusi vya Corona . 

Waziri wa Michezo alionyesha kwamba mkusanyiko wa harakati  utakaozinduliwa kwa wizara pamoja na  kushirikiana na Shirikisho la kimisri kwa Michezo ya kielektroniki, na vilabu vya afya,  utajumuisha shughuli na michezo kadhaa,  inayochangia kwa kiasi kikubwa kuongeza viwango vya afya na uzima wa mwili, na pia afya ya akili kati ya vikundi vyote vya jamii ya kimisri.


Hii inakuja kwa kuzingatia mpango wa wizara hiyo  unaolenga kujenga  mmisri kamili   katika nyanja zote za mwili, kisaikolojia, kiakili na kijamii na jukumu lake katika kutekeleza mkakati wa serikali katika uwanja wa michezo na vijana. Huduma hiyo inakamilisha mipango na miradi mingi inayolenga vikundi vyote vya watu wamisri "wanawake, waanzilishi, watoto, vijana. Watu wenye uwezo maalum "kwa kuzingatia Wizara ya Vijana na Michezo kuzindua Mradi wa Kitaifa wa uzima wa mwili na Afya, ambayo ni pamoja na mipango na shughuli zote zinazotekelezwa na Wizara hiyo kupitia lango la Misri kwa  Vijana na Michezo  na  mitandao ya kijamii.

Comments