Kuanzisha kituo cha mafunzo cha kimataifa ili kupambana na madawa ya kichocheo huko Misri

Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alipokea simu kutoka kwa mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la Kupambana na madawa ya kichocheo (WADA) Bwana (Witold Banka), Asubuhi ya leo, Alhamisi, simu imejumuisha majadiliano ya masuala mengi na mada nyingi.


Mwanzoni mwa simu , mwenyekiti wa Al-Wada alielezea shukrani zake na heshima kwa Waziri wa Michezo kwa msaada uliotolewa na serikali ya Misri kwa mfumo wa michezo barani Afrika, hasa katika uwanja wa kupambana na madawa ya kichocheo , pamoja na msaada wa serikali ya Misri kwa shirika la kupambana na madawa ya kichocheo ya Afrika (RADO), akiashiria kwamba alikuwa na hamu ya kuzuru Misri mara kwa mara na alikuwa amepangwa kuizuru Misri wakati wa miezi iliyopita na ziara yake ilichelewa kutokana na Corona , na pia alisifu jukumu la Dokta Ashraf Sobhy katika kuchukua mpango wa mkakati wa unaohusu wakala wa kimataifa wakati wa mkutano uliofanyika kupitia mkutano wa video, na Waziri wa Michezo alishiriki katika mkutano huo kwa sifa yake ya kimataifa kama mshiriki wa Ofisi ya kiutendaji ya  wakala wa kimataifa. 


Dokta Ashraf Sobhy, wakati wa mawasiliano marefu haya aliomba  mwenyekiti wa El-Wada  kuunga mkono wakala wa Kimataifa kwa hatua na taratibu hasa zinazopitishwa na Misri kupambana na madawa ya kichocheo , akiashiria dhamira ya serikali ya Misri kutoa na kuwezesha uwezo wote wa kumaliza taratibu za ruhusa kwa maabara ya kimisri, ambayo ilichelewa na Kamati Kuu ya wakala wa Kimataifa kwa sababu ya janga wa Corona ulimwenguni. 


Simu hiyo imejumuisha  majadiliano ya pendekezo lililowasilishwa na wakala wa Kimataifa wa uanzishaji wa kituo cha mafunzo na elimu katika uwanja wa kupambana na madawa ya kichocheo, iwekwe nchini Misri na kuwa moja ya vituo muhimu zaidi vya uhamasishaji na mafunzo kwa uwanja huu barani Afrika na Mashariki ya Kati, pamoja na kujadili maandalizi ya Michezo ya Olimpiki Tokyo 2021 na mipango ya wakala wa Kimataifa kuhusiana na Michezo mbalimbali na mipango ya uhamasishaji kabla na wakati wa michezo ya Olimpiki. 


Comments