Waziri wa Vijana na Michezo, alishiriki katika mkutano wa kimataifa wa "Michezo ni nguvu ya nchi na ujumbe wa amani"

Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alishiriki katika mkutano wa kimataifa wa "Michezo ni nguvu ya nchi na ujumbe wa amani" ulioandaliwa na Kitivo cha elimu ya Kimwili cha Chuo Kikuu cha Assiut, kupitia teknolojia ya mkutano wa video kutoka Juni 20 hadi 27 Juni, na ushiriki wa watafiti 600, katika kiwango cha ulimwengu wa Kiarabu.Mkutano huo unajumuisha kufanya mazungumzo matatu: "Michezo ni nguvu ya nchi na ujumbe wa amani", "michezo ya vyuo vikuu katika ulimwengu wa Kiarabu", na "Michezo na janga la Corona", ambapo hushiriki Dokta Tariq Abdullah Al-Jamal, Rais wa Chuo Kikuu cha Assiut, na Abd El-Moneim Amara, mkuu wa zamani wa Baraza kuu kwa Vijana na Michezo, Dokta Ali Al-Din Hilal, Waziri wa zamani wa Vijana, Dokta Kamal Darwish, Profesa wa Usimamizi na Mwenyekiti wa Kamati ya Sekta ya Masomo ya Kimwili, Dokta Ahmed Al-Minshawi, Makamu wa Rais wa Chuo Kikuu, na Dokta Jamal Muhammad Ali, mkuu wa kitivo na Rais wa Mkutano huo.Wakati wa uingiliaji wake, Dokta Ashraf Sobhy aliusifu mkutano huo na mada zake  zilizokuja kulingana na mtazamo wa kisayansi, kulenga ukweli wa michezo ya Kiarabu, wakati ambapo ulitokana na majadiliano ya jukumu la michezo kama moja wapo ya maeneo muhimu ambayo Rais Abd El Fatah El-Sisi aliizingatia "Usalama wa kitaifa."Sobhy aliongeza kwamba harakati za michezo za Misri zilishuhudia maendeleo ya kushangaza wakati wa miaka 6 iliyopita, akielezea kuwa serikali inalipa kipaumbele kubwa kwa uwanja wa michezo, na  mwaka wa 2019 ulikuwa mwaka maarufu katika suala la kupata matokeo na michuano katika michezo tofauti.


Na Sobhy aliisifu Misri kuwa Mwelekeo wa Mashirikisho ya kimichezo,na ikawa moja wapo nchi yenye kuvutia zaidi ulimwenguni kulingana na matukio, shughuli za kimichezo barani na nje,na hivyo kupitia miundombinu kubwa kwa michezo na vijana,na hilo linaakisi mchango wa Misri wa kukuza misingi ya Amani na huonyesha nguvu yake barani.

Comments