Esraa Younes ... mhitimu wa Shule ya Kiafrika, Mgombea wa Misri kwa Tuzo ya Kiongozi kijana mwafrika

Esraa Younes, mhitimu wa Shule ya Majira ya Kiafrika ya mwaka 2063, anashindana kwa tuzo ya Kiongozi kijana mwafrika, nayo ni tuzo inayotolewa na Taasisi ya " African Youth Architects" (AYA), kuwaheshimu viongozi vijana waafrika na kuzithamini juhudi zao katika kuunga mkono masuala ya bara la Afrika hasa yanayohusiana na vijana, na yanayohusu masuala kadhaa kama vile ( Jamii ya Kiraia, Uongozi, Mwanamke mwafrika, Amani na Mazingira) na kadhalika.

Nchi ya Morocco itapokea sherehe ya kuwaheshimu vijana walioshindana tuzo, wakati ambapo wagombea bora 30 walichaguliwa miongoni mwa wagombea 300 kwa tuzo hiyo - miongoni mwao ni mgombeaji mmisri Israa Younis - na ushindani wa tuzo hiyo ukawa juu ya ngazi ya kimataifa baada ya kutosheleza kwa kiwango cha Kiafrika.

Esraa aligombea tuzo kwa mpango wa "Kadroon Bikhtlaf", ambayo ni maadhimisho yaliyoandaliwa na Shirikisho la Michezo la Misri kwa Ulemavu wa Akili chini ya usimamizi wa Urais wa Jamhuri kila mwaka mnamo Desemba 24, ndani ya maadhimisho ya serikali kwa Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Ulemavu, na mpango huo unaangazia uwezo wa akili wa watu wenye ulemavu nchini Misri, Na uwezo wao mkubwa unaowatofautisha na wengine na kuonyesha mafanikio yao, pamoja na kutoa matarajio ya kufanikisha Ujihusishaji kati ya walemavu na jamii ili kushinda shida ya Uzembe ambapo watu wenye ulemavu huwekwa wazi katika shida hiyo, na uwezekano wa kuwashirikisha katika mchakato wa ujenzi wa jamii.

Esraa Younes, 26, amehitimu kutoka Kitivo cha Sheria, Idara ya Lugha ya Kiingereza, Chuo Kikuu cha Tanta, na akapata digrii ya uzamili katika sheria za kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Kairo, kisha akapata diploma ya tafsiri ya kisheria na tafsiri ya Umoja wa Mataifa kutoka Chuo Kikuu cha Marekani, pamoja na diploma mbili katika siasa na usimamizi wa shida kutoka kitivo cha Masomo ya juu ya kiafrika, chuo kikuu cha Kairo, naye sasa yuko katika hatua ya awali ya Uzamivu wake.

Esraa Younes alijitolea katika Ofisi ya vijana ya kiafrika katika Wizara ya Vijana na Michezo kama mtafiti mtendaji, na pia alifanya kazi kama mhadhiri katika Mfumo wa kuiga Umoja wa Afrika, pamoja na kazi yake kama mratibu wa vifaa katika Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Ulemavu "Kadroon Bikhtlaf", na pia alishikilia nafasi ya mkurugenzi wa mahusiano ya umma na nje katika Shirikisho la Michezo la Misri la Ulemavu wa akili.

Esraa ni mmojawapo wa viongozi wa mafunzo katika Taasisi ya Mafunzo ya Kitaifa, na aliiwakilisha Misri katika Mfumo wa kuiga mkutano wa kilele wa Kiarabu Kiafrika - katika Mkutano wa Vijana wa dunia, vilevile aliiwakilisha Misri katika mkutano wa kiwango cha juu nchini Botswana, mkutano ulioandaliwa na Umoja wa Afrika.

Kwenye kiwango cha bara, Israa alijiunga kufanya kazi kama mtafiti wa sheria katika Tume ya Haki na Ustawi wa Mtoto wa Tume ya Umoja wa Afrika ya Masuala ya kijamii.

Inatajwa kuwa Taasisi ya "AYA" ni Taasisi isiyo ya kiserikali, isiyohangaika faida, inayojali viongozi vijana waafrika wenye ushawishi mkubwa barani Afrika katika nyanja tofauti, wakati ambapo inalenga kuongeza misaada na ujasiriamali wa vijana barani Afrika, na hivyo kwa ajili ya kuunda bara lisilo na ukosefu wa ajira, umasikini na ujinga, kupitia Kuunga mkono mipango ya elimu na miradi ya maendeleo.Taasisi hiyo inatilia mkazo kwa utekelezaji wa Mpango wa kufanya kazi kwa vijana, Malengo ya Maendeleo Endelevu na Mpango wa hatua za Umoja wa Afrika 2063.
Ilianzishwa mnamo Machi 23, 2018, na iko nchini Gambia.

Comments