Waziri wa Michezo ashiriki katika sherehe ya (Raly ya Misri ) kwa Ujasiriamali katika Ligi ya Nchi za Kiarabu kupitia mikutano ya video

Kwa mahudhurio ya Bwana  Ahmed  Abo El Gheit, Katibu Mkuu wa Ligi ya ya Nchi za Kiarabu, Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alishiriki katika sherehe ya ligi ya Nchi za Kiarabu kwa uzinduzi wa Rally ya Ujasiriamali na Udhamini wa Mafunzo ya Ujasiriamali, kwa mahudhurio ya Dokta Khaled Abd El Ghaffar, Waziri wa elimu ya Juu,  Dokta  Nevin Jama, Waziri wa Biashara na Viwanda,  Dokta Ismail Abd El Ghaffar, Rais wa Chuo hicho, Mhandisi Hisham Okasha, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Al-Ahly, Dokta  Wael El Desouky, Mkurugenzi wa Kituo cha Ujasiriamali.


Wakati wa hotuba yake, Waziri wa Vijana na Michezo alitolea salamu kwa washiriki wote kutoka kwa mawaziri na maafisa waliosimamia sherehe hii, pia alimshukuru  Bwana Ahmed Abo El Gheit, Katibu Mkuu wa Ligi ya Nchi za Kiarabu, kwa mwaliko wake wa kuhudhuria sherehe hii, inayolenga kufungua milango na mitazamo  mipya kupitia ujasiriamali na kutoa fursa elfu 50 ya ajira kwa vijana wa Misri, zimetolewa na Chuo cha Kiarabu cha Sayansi na Teknolojia na usafiri wa bahari. 


 Sobhy ameongeza kuwa mkakati wa Wizara ya Vijana na Michezo unasisitiza maoni ya uongozi wa kisiasa katika kutoa fursa za ajira kwa vijana na jinsi ya kuwawezesha kupitia kushirikiana na taasisi na mashirika kadhaa ya kibinafsi, akionyesha kuwa wizara hiyo imetekeleza miradi na programu kadhaa ambazo hupewa vijana kwa kushirikiana na kifaa cha kuendelea miradi ya kati na midogo na midogo sana.


Sobhy alimaliza uingiliaji wake kwa kusisitiza jukumu bora lililochezwa na Ligi ya nchi za kiarabu inayoongozwa na Katibu Mkuu, Bwana Ahmed  Abo El Gheit, na Chuo cha Kiarabu cha Sayansi na Teknolojia na usafiri wa bahari, inayoongozwa na Dokta Ismail Abd El Ghaffar katika kusaidia uwanja wa ujasiriamali na kutoa fursa halisi kwa vijana wa Misri kwa kushirikiana na Benki ya Al-Ahly ya Misri inayoongozwa na Mhandisi Hisham Okasha.

Comments