Wardany .... Mwanachama wa Kamati ya kielimu ya Shule ya Kiafrika, apata Tuzo ya Nchi ya Uhamisishaji kwa 2020

Youssef Wardany – Msaidizi wa Waziri wa Vijana na Michezo kwa Masuala ya Vijana na mwanachama wa Kamati ya Taaluma ya Shule ya Kiafrika - alipata Tuzo ya Nchi ya Uhamisishaji katika uwanja wa Utamaduni wa kienyeji na msingi wa Usawa na kutobagua kwa mwaka 2020 kupitia kitabu cha "Ujuzi wa Kimataifa na kikanda katika Kupambana na Itikadi kali ", nacho ni kitabu kinachojadili moja ya masuala muhimu yanayoshikiliwa na makundi kadhaa ya kisiasa na kitaaluma ulimwenguni kote.

Kitabu hicho kinazungumzia uzoefu wa nchi 22 kutoka Ulaya, Afrika, Asia na Marekani Kaskazini, pamoja na uzoefu wa nchi kadhaa za Kiarabu, pamoja na Misri, katika uwanja wa kupambana na ugaidi, na kutokana na Uchambuzi wa uzoefu huo umesababisha umuhimu wa kuunda mkakati wa kitaifa unaohusika na kupambana na Itikadi kali kwa ushirikiano kati ya taasisi za nchi na Jamii ya kiraia, pamoja na hitaji la kuunda sera za haraka za kushinda shida zinazoikabili nchi, na utafiti huo ulitoa mtazamo wa kukabili mawazo yenye itikadi kali kwa kutegemea nguzo kadhaa, pamoja na elimu na mazungumzo ya jamii juu ya kupambana na Itikadi kali, pamoja na kuzindua mipango inayolenga kukuza Uelewa na kutekeleza njia ya kielektroniki, na kuanzisha vituo maalum vya fikra ; kupambana na Itikadi kali.

Youssef Wardany anazingatiwa mtafiti mhusika katika masomo ya vijana na kupambana na Itikadi kali, amezaliwa mnamo 1981, alihitimu kutoka kwa Kitivo cha Uchumi na Sayansi za kisiasa, Chuo Kikuu cha Kairo 2002, na akapata digrii ya Uzamili katika haki za binadamu kutoka kwa Shule ya London kwa Uchumi na Sayansi za kisiasa mnamo 2009, kisha akapata diploma katika sera za umma na haki za watoto Kutoka kwa Kitivo cha Uchumi na Sayansi za kisiasa mnamo 2013, pia alipata digrii ya Uzamili katika Mafunzo ya Ulaya kutoka Kitivo cha Uchumi na Sayansi za kisiasa , Chuo Kikuu cha Kairo kwa kushirikiana na Taasisi ya Sayansi za kisiasa nchini Ufaransa na vyuo vikuu viwili vya Berlin na Barcelona -2014, naye sasa ni mtafiti wa Uzamivu katika masomo ya Euro-Mediterranean.

kwa upande wa uzoefu wa kitaalam na kazi, Wardani alifanya kazi kama mtafiti katika Ofisi ya kiufundi ya Waziri wa Vijana kutoka 2003 hadi 2013, kisha akawa Msaidizi wa Waziri wa Vijana na Michezo kwa Masuala ya Vijana mnamo 2014, na tangu 2018 akawa Msaidizi mkuu wa Waziri wa Vijana na Michezo kwa Masuala ya Vijana.

Pamoja na hayo, Yousef Wardani alifanya kazi kama mratibu wa kitaalam wa mpango wa semina za mafunzo kwa taasisi ya kidiplomasia ya Wizara ya Mambo ya nje ya kimisri mnamo 2015. Naye alikuwa mwanachama wa ujumbe wa kimisri uliotoa juhudi za Misri katika uwanja wa kupambana na Itikadi kali wakati wa Ziara ya Kamati ya Kupambana na Ugaidi ya Umoja wa mataifa mjini Kairo mnamo Julai 2017. Pia alikuwa mwanachama wa Kamati ya Utamaduni wa Uraia na Haki za Binadamu kwenye Baraza Kuu la Utamaduni kutoka 2017 hadi 2019.

Youssef Wardany alichangia kuunda mkakati wa vijana nchini Misri, na aliiwakilisha serikali ya Misri katika karibu na mikutano ya kimataifa 12.

pamoja na ushiriki wake kama mtaalam katika shughuli za Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, Tume ya Uchumi ya Umoja wa mataifa barani Afrika, ofisi ya kikanda ya UNESCO huko Beirut, na vituo kadhaa vya mawazo vya kimataifa, pia alifanya kazi kama mwenye uamuzi wa mikutano ya vijana Waarabu iliyoandaliwa na Maktaba ya Aleskandaria katika kipindi cha kuanzia 2006-2011, na kupata kwake kwa Ushirika wa Baraza la Kitaifa la Uongozi na Vijana huko Marekani mnamo 2013, na kuanzisha Jukwaa la Safwa mnamo Februari 2019.

Wardaغi alipokea Udhamini na tuzo kadhaa, ikiwa ni pamoja na kupata nafasi ya kwanza kwa kiwango cha vyuo vikuu vya kimisri kupitia utafiti wa jina la "Kuzima Uyahudi huko Yerusalemu na haki ya kuamua hatima", Juni 2002. Pia alishinda nafasi ya pili katika Mashindano ya Taasisi ya Kiarabu ya Mafunzo, Utamaduni na Sayansi kwenye Ligi ya Nchi za Kiarabu kwa utafiti uliopewa kichwa cha "Sera za Ujihusishaji wa Vijana Waarabu: Mtazamo na Tathmini", Novemba 2016.

Mnamo 2020, shughuli zake za hivi karibuni zimefikia tuzo ya Nchi ya Uhamisishaji katika uwanja wa utamaduni wa kijadi na msingi wa Usawa na kutobagua.

Tuzo za Nchi za Uhamisishaji zinazingatiwa moja ya tuzo zinazotolewa na nchi kwa watu bora katika nyanja tofauti, nazo ni tuzo 40 zilizosambazwa kama ifuatavyo (tuzo 11 katika uwanja wa sayansi za kimsingi - tuzo 10 katika uwanja wa sayansi za kilimo - tuzo 9 katika uwanja wa sayansi za tiba - tuzo 10 katika uwanja wa sayansi za uhandisi. ), Na thamani ya kila tuzo ni paundi elfu hamsini, kwa kuzingatia kutoruhusa kupewa zaidi ya mara moja kwa mtu mmoja isipokuwa baada ya kupita miaka mitano tangu kupata tuzo hiyo kwa mara ya kwanza, pia hairuhusiwi mtu mmoja kupata tuzo hiyo zaidi ya mara mbili katika uwanja mmoja, na Haki ya kutangulia kwa tuzo hizi ni kwa watu binafsi tu.

Comments