Waziri wa Michezo ashiriki katika mkutano wa shirikia la Kimataifa la Kupambana dawa za kusisimua misuli kupitia mikutano ya video

Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alishiriki katika mkutano wa Bodi ya shirika  la Kimataifa ili Kupambana dawa za kusisimua misuli  " WADA " kama mjumbe wa mkutano , kupitia teknolojia ya  mikutano ya video  kwa mahudhurio ya wajumbe wa Bodi ya shirika, imeongozwa na Whitold Banca, na wanachama  wa Bodi ya Shirika la taasisi ya barani Afrika, na Mwenyekiti wa Tume ya masuala ya Mambo ya Jamii katika Umoja wa Afrika.


Mkutano huo ulijadili njia za kuunga mkono kwa Shirika la Kimataifa la Kupambana na Dawa za kusisimua misuli  kutekeleza mipango na mikakati yake  ulimwenguni kwa kushirikiana na mashirika ya kitaifa ya kupambana Dawa za kusisimua misuli kwa kuzingatia hali ya kisasa na maendeleo ambayo yameathiri mfumo wa michezo kutokana na mzozo wa Corona, pamoja na vifaa na maandalizi yanayohusiana na kuandaa michezo ya Olimpiki ya Tokyo na kikao cha Michezo ya Paralympiki ya mwaka ujao.


Kwa upande wake, Dokta Ashraf Sobhy alipendekeza kuundwa kwa kamati maalum ili kutafuta njia maalum za kuboresha rasilimali za Shirika la Kimataifa Kupambana na dawa za kusisimua misuli  kwa njia  inayochangia kuongeza uhuru wa uamuzi wa WADA, na inashikilia uadilifu wa mfumo wa kupambana wa dawa za kusisimua misuli   ulimwenguni.


Wanachama wa Al-Wada walikubaliana kuendelea na majadiliano kuhusu kutoa msaada unaohitajika kwa shirika hilo kutekeleza jukumu lake kikamilifu, na kufuata na mashirika ya kitaifa ya kupambana dawa za kusisimua misuli  kutekeleza mipango mbalimbali ya uhamasishaji na mipango ya mashirika inayohusiana na michezo tofauti.

Comments