Timu ya taifa ya Misri iko katika uainishaji wa pili wa kura ya kombe la dunia la mpira wa mikono 2021

Shirikisho la kimataifa la mpira wa mikono limeweka viwango vya timu za kitaifa kabla ya kuanza kwa kura ya michuano ya dunia ya mpira wa mikono ( Misri 2021), na iliyopangwa kuifanyika mnamo mwezi wa Januari ujao, na timu ya kitaifa ya mafarao imekuja katika uainishaji wa pili.


Kombe la dunia la mpira wa mikono litafanyika kwa mfumo mpya na litashuhudia ushindani wa timu za kitaifa 32 kwa mara ya kwanza, timu hizo zimegawanywa kwenye vikundi vinane, kila kikundi kinajumuisha timu nne ambazo zimegawanywa kwa kumbi 4 zinazokaribisha michuano mnamo kipindi cha tarehe 13 hadi 19 Januari.


Uainishaji wa timu za kitaifa umekuja kama ifuatavyo :


- Uainishaji wa kwanza : Denmark, Uhispania, Kroatia, Norway, Slovenia, Ujerumani, Ureno, Uswidi.


- Uainishaji wa pili : Misri, Argentina, Tunisia, Algeria, Qatar, Austria, Hungary, Belarusi. 


- Uainishaji wa Tatu : Iceland, Brazil, Ufaransa, Korea Kusini, Japan, Bahrain, Jamahuri ya Czech, Uruguay. 


- Uainishaji wa nne : Angola, Cap Verde, Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Morocco, Poland, Urusi + timu ya kitaifa kutoka kwa bara la Marekani ya Kusini + timu ya kitaifa kutoka kwa bara la Marekani ya Kaskazini. 


Na timu 3 za kitaifa za kwanza kutoka kwa kila kikundi zimefikia duru kuu ( timu za kitaifa 24 ) ( mnamo kipindi cha tarehe 20 hadi 25 Januari ), huku timu ya kitaifa ya mwisho ya kila kikundi itacheza juu ya kombe la Rais ( mechi za heshima ili kubaini nafasi kutoka 25 hadi 32 ). 


Timu 24 za kitaifa zinazofikia  duru kuu zitagawanywa kwa vikundi vinne, kila kikundi kinajumuisha timu 6, timu ya kitaifa ya kwanza na ya pili zinafuzu zamu ya 8 , zamu itakayochezwa kuanzia siku ya 27, kisha nusu ya fainali itakayochezwa siku ya 29, na fainali itacheza katika siku 31 Januari. 


 Michuano ya kombe la dunia la mpira wa mikono la wanaume inazingatiwa michuano mikubwa zaidi ya michezo hiyo, na itakaribishwa na Misri mnamo mwaka ujao kwa ushiriki wa timu za kitaifa 32 duniani kote, na mashabiki wanatarajia kuwa Misri inashinda katika Michuano medali ya kidhahabu, baada ya mafanikio makubwa yaliyohakikishwa na Timu ya kitaifa ya wavulana na kuhamasisha mashabiki kwa kushinda lakabu ya kombe la dunia la mwisho huko Macdonia. 

Comments