"Nembo ya Al-Ahly" iliundwa na mjomba wa mfalme na ilibadilika mara 3

Kila Kilabu kina nembo yake inayotofautisha na kuelezea tabia na sera yake, na kwa sababu Kilabu cha Al-Ahly kilikuwa kiongozi barani Afrika, nembo yake ilikuwa ina umuhimu wenyewe kati ya vilabu vya kimataifa, wakati gazeti la Uhispania Marca likilichagua kama nembo bora kwa kilabu ulimwenguni, na mtu wa kwanza aliyeunda nembo ya kilabu hiki alikuwa Bwana Sharif Sabry, aliyekuwa akifanya kazi kama mwanachama wa kamati ya kiutendaji tangu mwaka 1916 hadi 1923 na pia mwanachama wa baraza la uongozi katika Kilabu cha Al-Ahly na Kamati Kuu mnamo mwaka 1926, huku sheria ya kilabu hiki kiliwekwa na Bwana Abdul Khaleq Tharwat pasha. 


Muhammad Sharif Sabry mwenye  asili ya Uturuki , alikuwa kaka wa Mfalme wa Misri (Nazli) , na mjomba wa Mfalme Farouk, na "Sabry" aliunda nembo ya kilabu katika siku ya 3 Novemba, mwaka 1917, ili kuwa nembo ya kwanza ya Al-Ahly.


Kilabu cha Al-Ahly kilipata nembo yake ya kwanza kutoka kwa rangi ya bendera ya Misri , na ilikuwa bendera ya Ottoman ( Uturuki ) wakati wa utawala wa mtawala Abbas  Helmy wa pili, bendera hiyo ilikuwa iliyojumuisha hilali na nyota ndani ya hilali hiyo, na rangi za shati zilikuwa nyekundu na nyeupe, na ziliendelea kwa nusu nyekundu na nusu nyeupe, na nembo ya Klabu hiyo imepambwa kwa taji ya mfalme, ambayo ni ishara ya utawala hapo juu, na mwisho wa chini uliandika jina la Al-Ahly, na katikati ya tai anayeruka, ndege huyu mkubwa aliyekuja kama ishara ya afya na pia ishara ya kuruka na kuchochea.


Baada ya mapinduzi ya 1952, alama ya nchi ilibadilishwa kutoka taji kuwa tai, taji ilichukuliwa kutoka nembo yake, na iliendelea hadi 2007 ili  kufanya mabadiliko kadhaa tangu wakati huo kusherehekea karne kwa kubadilisha sura ya tai na kuongeza jina la Al-Ahly kwa Kiingereza na mwaka wake wa kuanzisha .


Wakati wa sherehe ya karne moja ya kilabu cha Al-Ahly, nembo hiyo ilibadilishwa, tai na njia ya kuandika Al-ahly kwa Kiarabu hapo juu na kwa Kiingereza na tarehe ya kilabu katika chini, na kuweka nyota tatu juu ya nembo na kila nyota kuashiria mashindano ya ligi kumi ya Misri ambayo yameongezwa hivi karibuni kwenye nyota ya nne ya nembo juu yake, na chini ya nembo kuweka idadi ya nyota kwa idadi ya mara za kushinda michuano ya Afrika, ambayo Al-Ahly imeishinda mara 8 hapo awali.Comments