Kujiandaa kwa Kombe la Dunia la mpira wa mikono , Wizara ya Vijana yazindua taarifa ya habari kwenye tovuti ya kielektroniki kwa lugha 4


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alikubali kukuza mfumo wa tovuti ya kielektroniki ya wizara hiyo, "Lango la Misri la Vijana na Michezo", ili kuzinduliwa rasmi kwa lugha nne ( Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa na Kiswahili ), hii katika kuandaa kwa  Kombe la Dunia la mpira wa mikono litakalokaribishwa na Misri mnamo Januari ijayo, na pia kwa ajili ya mawasiliano na vijana ndani na nje ya Misri.


Dokta Ashraf Sobhi, Waziri wa Vijana na Michezo, alisisitiza kwamba tovuti ya kielektroniki ni mfumo kamili wa vyombo vya habari uliojumuishwa (tovuti ya habari - idhaa ya mtandao - kituo cha Youtube - kurasa za Facebook, Twitter na Instagram) zinazohudumja  vijana wa Misri ndani na nje ya nchi na kuwa njia ya mawasiliano kati ya vijana wa Misri na vijana wa ulimwengu.


Waziri wa Michezo ameongeza kuwa wizara yetu, itafanya kazi ya kutoa huduma mpya kwa Mashindano ya Kombe la dunia la mpira wa mikono  yatakayofanyika nchini Misri na kutolewa kwa lugha nne ili kuelezea kile kinachotokea katika viwanja vya mashindano na kutoa huduma kwa mashabiki mahali popote.


Aliongeza kuwa nchi ya Misri inafanya juu chini kwa ajili ya  mafanikio ya mashindano haya katika nyanja zote, na vyombo vya habari ndiyo njia karibu zaidi ya kufanikisha mafanikio kwenye hakika , na kwa hivyo tutatoa huduma nyingi kwa wageni wa Kombe la Dunia kabla, wakati na baada ya mashindano. Kwa kuongezea huduma zinazotolewa na serikali kuonyesha mahali na nafasi ya Misri duniani .


Akionesha kuwa hii inakuja katika mfumo wa  huduma zinazotolewa na wizara hiyo ili kufanikisha Kombe la Dunia kufanikiwa ambayo ulimwengu wote unangojea kuonesha uwezo wa Misri kuandaa mashindano ya ulimwengu, kama mafanikio katika kuandaa hafla mbili kubwa barani Afrika, Mashindano ya Mataifa ya Afrika na fainali za Kiafrika zinazofikiwa  Olimpiki, ambapo tovuti hiyo itazinduliwa kwa lugha nne ili kuwasiliana na vijana katika mahali popote, aliongeza kuwa tovuti ya kielektroniki haitakuwa tu na kutoa huduma za michezo, kutoa taarifa  za mashindano ,  mazungumzo ya mabingwa na habari zao tu, lakini inaenea kwa kutambua timu, mashindano, mahali na jinsi ya kuhudhuria mechi, na kutoa vivutio vya utalii na vya akiolojia ambavyo ziko katika mikoa sita itakayokaribisha vikundi sita vya michuano , Tovuti pia itatoa huduma ya picha  bure kwa ufanisi mkubwa, na inapatikana kwa vyombo vyote vya habari vya kitaifa na kimataifa.


Imepangwa kuwa Redio ya Vijana ya Misri inayohusiana na Wizara ya Vijana na Michezo itatolewa kwa ajili ya kuzingatia  michuano wakati wote .. Kundi la watangazaji wapya na wasomaji wa habari hivi sasa wanapewa mafunzo ya kuanza redio katika mfumo wake mpya pamoja na hafla ya kura , na pia mafunzo ya vijana waume na wanawake 25 kutoka vyuo vikuu vya Vyombo vya habari na wahitimu wake na wanafunzi wenye vipaji kutoka vyuo vingine kuwa msingi wa watangazaji wa siku zijazo na kitu kipya kilichotolewa na Wizara ya Vijana kwa vyombo vya habari vya Misri.


Tovuti ya kielektroniki ya Wizara ya Vijana na Michezo imeshuhudia maendeleo ya kushangaza mnamo kipindi kilichopita ambapo imekuwa njia kamili ya vyombo vya habari ya kuingiliana na vijana na ni nyumba na kituo kwao kwa suala la huduma zinazotolewa na wizara hiyo, na pia kuwa njia ya mawasiliano na vijana nje ya nchi, ikiwa wanaoishi nchini Misri au wahamiaji ili kujua Misri kwa ndani katika masuala yote ,mahala pa kiutalii, huduma na mashindano ambayo Misri inashiriki ndani yake.

Comments