Chini ya kauli mbiu " Mchezo wako .. Kinga yako " .. Waziri wa Michezo ashiriki vijana 500 katika Mashindano ya baiskeli

Dokta Ashraf Sobhy Waziri wa Vijana na Michezo alishiriki katika Mashindano ya Baiskeli yaliyopangwa na wizara ya vijana na michezo leo saa  moja na nusu asubuhi chini ya kauli mbiu ya " Mchezo wako.. Kinga yako " kwa mahudhurio ya wavulana na wasichana  500 miongoni mwa wale waliopata Baiskeli kwenye mpango wa " Baiskeli yako .. Afya yako " uliozinduliwa na Wizara hivi karibuni.  


Mashindano hayo yalizinduliwa kutoka kwa lango la Stadi ya Kairo ya Kimataifa , barabarani Yosef Abas mbele ya kituo cha utabibu cha kiarabu , ikipita njia ya Tayaran na daraja la  Shahidi Hesham Barakat kisha kurudi mwanzoni ambapo umbali ni karibu kilomita 5 mnamo wakati wa nusu saa .


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa vijana na michezo akaelezea kuwa Mashindano yanakuja kama moja ya shughuli za kimchezo  zinazoangaliwa na Wizara ya vijana na michezo kupitia mpango wa " Baiskeli yako .. Afya yako ", na kulingana na maelekezo ya uongozi wa kisiasa ili kueneza utamaduni wa kufanya mazoezi , na kwenye mfumo wa kutekeleza moja ya mihimili ya mkakati wa wizara inayowakilisha katika kuufanya mchezo mtindo wa maisha , na kuwahamasisha wananchi kufanya mazoezi .


Akiongeza kuwa mpango utaendelea katika mikoa yote ya Jamuhuri kupitia awamu ijayo , akiwashukuru vijana wote wanaoshiriki , wakilazimika shughuli zote za kujikinga ili kupambana na virusi vya Corona wakati wa ushiriki katika Mashindano. 


Sobhy akaashiria kwamba Wizara inashughulikia mipango kadhaa mbalimbali inayolenga kusambaza mchezo ndani ya jamii kwa ushirikiano wa taasisi maalumu , hiyo kwa ajili ya usambazaji  wa kufanya mazoezi kati ya wananchi , kutekeleza maelekezo ya uongozi wa kisiasa kuufanya mchezo kitu muhimu maishani mwa mwananchi mmisri , kuzingatia umuhimu wake kwa pande zote za kimwili na kiafya.

Comments