Kuahirishwa kwa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa na kombe la Konfedralia kwa wiki tatu

Kamati ya kiutendaji ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF)  katika mkutano wake imeamua kuahirisha nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Konfedralia kwa wiki tatu.


Mechi ya kwenda ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa inatarajiwa kuchezwa mnamo tarehe 16 na 17 Oktoba ijayo, na mechi ya kurudi itakuwa wiki moja baadaye, na kisha fainali itafanyika mnamo Novemba 6.


Kuhusu Kombe la Shirikisho la kiafrika"Konfedralia" , Morocco itakaribisha nusu fainali ya raundi moja mnamo 19 na 20  Oktoba, na fainali itafanyika tarehe 27 Oktoba .


Kwa kuanza kwa msimu ujao, kutakuwa mnamo Novemba 27, kwa kucheza mechi za raundi za awali za mashindano hayo mawili.

Comments