Wasichana bora katika michezo ya kimisri ... Uwatambue

Michezo ya Misri inashuhudia katika kipindi cha kisasa zaidi ya hodari  wa michezo katika michezo tofauti , kama  mpira wa kikapu, karate,  mchezo wa kunyanyua chuma , tenisi ya meza, na michezo mingine, khususana mingoni mwa  , na kulingana na mafanikio yaliyofanywa na wachezaji hawa kwenye mchezo wanaofanya mazoezi, ikiwa kwa kiwango cha Kiafrika au cha kimataifa, kwa hivyo wanaitwa "mashujaa", haswa kwani wamepata mafanikio ambayo hayajawahi kupatikana hapo awali na mtu yeyote katika mafanikio yao. Miongoni mwa wasichana hawa ni Farida Othman, Hana Guda, Soraya Muhammad, Fatma Omar, na Giana Farouk.

Fatma Omar


Bingwa Fatma Omar, bingwa wa mchezo wa kunyanyua chuma wa paralympiki , ndiye mchezaji wa kwanza katika historia ya Misri, Afrika na ulimwengu wa Kiarabu kupata medali 5 katika mashindano 5 ya Olimpiki mfululizo, kuanzia Sydney 2000 hadi Rio 2016, pamoja na dhahabu nne mfululizo. Alichaguliwa kuwa mchezaji bora zaidi ya mara moja katika rekodi za Kamati ya Kimataifa ya Walemavu katika 2012, mwenye rekodi ya ulimwengu akiwa na kilo 56, na uzani wa kilo 142. Alivunja rekodi ya Olimpiki na ya ulimwengu na alisajiliwa kwa jina lake, na Fatma Omar anachukuliwa kama ishara ya kuinua uzito, sio tu kwa kiwango cha Kiarabu na Kiafrika, bali pia Duniani.


Hana Goda


Hana Goda mchezaji wa timu ya ya taifa kwa tenisi ya meza aliyeweza kumuwekea nafasi kati ya watu wazima, baada ya kushinda ubingwa na mataji yake mengi  na taji la mwisho  lililotolewa na viwango vya juu ulimwenguni kulingana na Shirikisho la Kimataifa kwa mara ya tatu mfululizo, na kabla yake kushinda dhahabu kwenye Mashindano ya Ureno ya Kimataifa kwenye mashindano ya Vijana chini ya miaka 12 na 15, na shaba katika Mashindano ya Shirikisho la Dunia kwa mabara katika mafanikio ambayo hayajawahi kutokea katika historia ya tenisi ya meza ya Misri, na kwa kiwango cha kitaifa alifanikiwa kushinda Mashindano ya Wanawake wa Jamuhuri kwa kumpiga mchezaji wa klabu ya Zamalek ambaye ana umri wa miaka 27, wakati Hana ana miaka 12 tu.


Farida Othman


Farida Othman mchezaji katika timu ya taifa kwa kuogelea alishinda medali ya shaba katika mbio za kipepeo za mita 50 wakati wa ushiriki wake kwenye mashindano ya ulimwengu  yaliyofanyika nchini Hungary mnamo Agosti iliyopita, kuwa mwogeleaji wa kwanza wa Misri kufikia mafanikio haya, kisha alishinda tuzo ya mwanariadha bora wa kike barani Afrika kwa mwaka 2019 pia, pamoja na kushinda Tuzo ya Mohammed bin Rashid Al Maktoum ya Ubunifu wa Michezo, Dhahabu ya bahari ya kati  na dhahabu ya Michezo ya kiafrika.


Soraya  Muhammed


Mchezaji wa mpira wa kikapu kwenye klabu ya Al-Ahly na mchezaji wa timu yataifa pia amepata michuano kadhaa , pamoja na ubingwa wa Kiarabu katika kiwango cha timu ya kitaifa na kutawazwa na klabu yake kwa shaba katika Mashindano ya Afrika ya klabu  yaliyoandaliwa na Misri, na pia kutwaa na timu ya kitaifa katika Ubingwa wa Kombe la Afrika 3/3 huko Uganda, na kushinda taji la mchezaji bora zaidi Katika Kombe la Afrika huko Uganda,  alishinda taji la mfungaji bora katika michuano ya afrobasket baada ya kufikisha alama 85, na kutawazwa tuzo ya mfungaji bora katika Kombe la Mataifa ya Afrika lililopita huko Senegal . Alielezewa kama Cleopatra wa mpira wa kikapu na Shirikisho la Kimataifa la Mchezo na alichaguliwa kati ya wachezaji 10 bora ulimwenguni mwaka 2019 na Shirikisho la Kimataifa la mpira wa kikapu.


Giana Farouk


Giana Farouk mchezaji wa Karate na bingwa wa ulimwengu aliweza licha ya umri wake mdogo kupata ubingwa na mataji mengi, akifikia medali 7 za dhahabu kwenye mashindano ya ulimwengu na medali 13 za dhahabu katika mashindano mengine ya kimataifa pamoja na medali 15 za fedha ,pia alifikia Olimpiki ya Tokyo awe Mmisri wa kwanza, Mwarabu na Mwafrika kufanikiwa  kufikia olimpiki, haswa kwani toleo hili ni la kwanza ambalo mchezo wa karate unashiriki .

Comments