Kocha wa timu ya taifa ya Uswidi: kuchagua Misri kunatuhimiza, na ninadhani kuwa sisi ni bora zaidi katika kikundi chetu

Kocha wa timu ya taifa yaUswidi “Glenn Solberg ” anaona kuwa timu yake lazima kuwa timu bora zaidi  katika kikundi chake katika toleo la 27 kutoka mashindano ya dunia ya mpira wa mikono ya wanaume- Misri 2021.


Timu ya taifa ya Uswidi iliyoshinda mashindano kwa mara nne kabla ya hivyo iliwekwa  katika kikundi cha saba, pamoja na timu ya Misri –mwenyeji -, timu ya Ucheki, na timu ya kuiwakilisha  Marekani kusini -itakayochukuiwa baadaye.


Mswidi Solberg amesema: “kukabili timu ya Misri nchini Misri ni jambo gumu, lakini kuchahuliwa kwao kwa kucheza dhidi yetu ni jambo linalotuhimiza”.


Akaongeza: “jambo linategemea kwenye msimamo wa kuhudhuria kwa watazamaji. Kucheza katika ukumbi unaojaa na watazamaji mjini  Kairo bila shaka litakuwa jaribio zuri sana”.


Akakamilisha: “pia, timu ya Ucheki ina wachezaji wanaovutia, na imepata kiwango cha sita katika mashindano ya mataifa ya Ulaya, mwaka 2018”.


Akasisitiza: “kila kikundi kina timu mbili au tatu  nzuri sana, lakini ninadhani kuwa timu yetu lazima kuwa bora kuliko zote”.


Ama Mkuu wa timu “Jim Gotfreidson” amesema: “ninapenda kucheza mashindano ya kikundi, na ninataka kuiwakilisha Uswidi nchini Misri”.


Akakamilisha: “kucheza dhidi ya Misri kwenye ardhi yake na jaribio zuri sana, na ninadhani kuwa fainali ya kikundi itakuwa baina yetu na timu ya Misri”.


Akahitimisha: “pia, tuna heshima kubwa kwa timu ya Ucheki”.

Comments