Waziri wa Michezo wakati wa kukagua kwake kwa ukumbi uliofunikwa huko Uwanja wa Kairo

Kura ya Kombe la Dunia imezidi utazamaji bilioni

Waziri wa Vijana na Michezo, Dokta Ashraf Sobhy alisisitiza kuwa utazamaji wa sherehe ya kura ya Mashindano ya Mpira wa mikono ya Dunia ulizidi utazamaji bilioni moja kutoka nchi tofauti za Dunia.


Hii ilikuja wakati wa ziara ya ukaguzi ambayo Waziri wa Michezo aliifanya katika ukumbi mkuu uliofunikwa wa Uwanja wa Kairo, akifuatana na Dokta Hassan Mustafa, Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Mikono la Kimataifa,  Jenerali  Ihab El-Far, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Uhandisi, na Jenerali Ali Darwish, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Uwanja wa Kairo.


Waziri huyo, Dokta  Ashraf Sobhy alisisitiza kuchukua hatua zote za tahadhari za kukabiliana na virusi vya Corona wakati wa mashindano kwa uratibu wa  kamati ya matibabu iliyoundwa na Shirikisho la Kimataifa kwa mpira wa mikono , mamlaka na Taasisi husika nchini Misri.


Ukumbi mkuu uliofunikwa unaoweza kuchukua mashabiki 22,000, unakaribisha mechi za kundi la nne,linalojumuisha Misri , Uswidi, Ucheki na mwakilishi wa Marekani Kusini, na mechi za kundi la nne zinazojumuisha Denmark, Argentina, Bahrain na Congo ya Kidemokrasia.

Comments