Waziri wa Vijana na Gavana wa Aleskandaria wapo katika mazungumzo wazi pamoja na vijana wa Misri

Pembezoni mwa mkutano wa duru ya kwanza ya Bunge la watoto wa Misri..Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na michezo, na Meja Jenerali Mohammed El-Sharif, Gavana wa Aleskandaria, walikutana na idadi kadhaa ya vijana kwenye mikoa ya Jamhuri katika mazungumzo wazi kwenye ukumbi wa mji wa vijana huko Aleskandaria, hivyo pembezoni mwa mwanzo wa mkutano wa duru ya kwanza ya Bunge la Watoto  wa Misri.


Shughuli za mkutano zilianza na maonyesho ya maandishi, yanajumuisha kuonyesha miradi, programu na mipango ya baadaye kwa Wizara ya Vijana na michezo, maonyesho hayo yalitolewa na wakuu wa utawala mkuu kama Meja Jenerali Ismail El-far, Mwenyekiti wa idara kuu ya Ajira ya Vijana, na Bibi Dina Fouad, Mwenyekiti wa idara kuu ya Bunge na Elimu yaa kiraia, na Bibi Najwa Salah, Mwenyekiti wa Idara kuu kwa programu za kiutamaduni na ufahamu.


Mwanzoni mwa kauli yake, Dokta Ashraf Sobhy, Waziri huyo alisisitizia kuunga mkono kwake kamili kwa vijana kupitia jukumu lao linaloonekana na Misri kwa kushiriki na kujithibitisha katika nyanja za kuimarisha na ujasiri wao katika kufungua upeo mpya kwa kuwekeza fursa kwa ujuzi na kujifunza utawala  unaojumuisha Demokrasia nzito na kali na kuwekeza fursa muhimu ili kufanikisha Demokrasia.


Alielezea  kuwa ujumbe wa Wizara ya Vijana na michezo unazinduliwa kupitia uunganishi kati ya Wizara mbalimali, nchi ina changamoto ya kupambana na shida, uongozi wa kisiasa unashughulikia usawa katika nyanja zote kwenye mikoa tofauti ya Misri ili kukuza rasilimali za watu kisayansi ili kukabiliana na changamoto, tunaunga mkono utofauti katika mfumo wa elimu na pia kuunga mkono kwa shughuli za wanafunzi katika vyuo vikuu na vyuo vya juu.


Waziri huyo ameongeza kuwa Misri katika kiwango cha michezo ilifanikiwa kuandaa na kukaribisha kombe la Mataifa ya Afrika 2019, na pia kuandaa Kombe la Dunia la Mpira wa Mikono Januari ijayo, aliashiria kuwa sherehe ya Ufunguzi wa mashindano hayo ilishinda sifa duniani, akionesha kuwa sura ya Misri imetofautiana vyema Ulimwenguni mnamo mahudhurio ya Rais Abd El-Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, akielezea kwamba Misri haikukusudiwa kuwa nchi yoyote, lakini Misri ilifanikiwa kukabiliana na majaribio hayo yote.


Kwa upande wake, Gavana wa Aleskandaria Mohammed El-Sharif alisema, "kizazi cha kisasa cha vijana ni bora zaidi kuliko chetu, ni kizazi kinachoweza kuwa na bahati nzuri kuliko vizazi vilivyopita kwa sababu ya maendeleo makubwa ya kiteknolojia, vijana ni kiini cha siku zijazo na tumaini ambalo litasukuma Misri mbele, alisisitiza kuwa Misri imejaa na vijana na nguvu zinazoweza kuendeleza maendeleo.


Kujibu maswali ya vijana juu kuwepo kwa Aleskandaria katika kiwango cha kwanza cha ukiukaji, alizumgumzia  sheria ya suluhu katika ukiukaji, akiashiria kuwa Aleskandaria ina zaidi ya maamuzi 13,000 ya kuondoa, lakini elfu chahe tu ambazo zimetekelezwa, alisisitiza kuwa serikali zinazofuatana, licha ya nguvu zao, lakini hazijaweza kukomesha ukiukaji huu kabla ya Rais Abd El-Fatah El-Sisi ataingilia kati na kutoa maagizo yake ya kushughulikia jambo hilo kwa ukali na umakini, akielezea kuwa bila mhimili wa Mahmudiyah, Aleskandaria ilikuwa imepooza kabisa tangu miaka, akiongeza kuwa mhimili wa Mahmudiyah ni ateri ya kuokoa tumaini na maisha mkoani Aleskandaria.

Comments