Waziri wa vijana na michezo azindua ishara ya kuanza kwa mashindano ya pikipiki ya Misri

Dokta Ashraf Sobhy Waziri wa vijana na michezo alizindua jumamosi mchana ishara ya mashindano ya pikipiki ya Misri kwa kuhudhuria kwa Dokta Ibrahim Elshehabh Naibu Gavana wa mkoa wa El _Giza  , Bwana Omar Heredy mkuu wa shirikisho la kimisri la pikipiki , Dokta Amr Elhadad Msaidizi wa Waziri wa vijana na michezo kwa maendeleo ya kimichezo na Dokta Ahmed Gomaa mshiriki wa Waziri kwa maendeleo ya kimichezo . 


Sobhy alielezea furaha yake kwa kuzindua ishara ya mwanzo katika mashindano , akibainisha kuwa Misri ipo tayari sana kupokea michuano mbalimbali na Wizara inachukua tahadhari zote za kujikinga na virusi vya Corona , akisisitiza kuwa wote wanashirikiana pamoja kwa ajili ya kuonesha matukio yote kwa sura inayofaa nafasi ya Misri katika jamii ya kimataifa . 


Akiongeza kuwa kurudi kwa shughuli za mashindano ni hatua muhimu katika kukamilisha kurudi kwa shughuli na miradi ya michezo inayoakisishwa kwa sura nzuri  katika sekta mbalimbali za nchi , hususan za utalii na uchumi kwa jumla .

Comments