"CAF" yaelezea kupendeza kwake kwa wimbo wa kitaifa wa Misri kati ya mashabiki elfu sabini

 Shirikisho la kiafrika la Soka (CAF) lilielezea  kufurahishwa kwake kwa wimbo wa kitaifa wa Misri, ulioimbwa na zaidi ya mashabiki elfu sabini kwenye uwanja wa kimataifa wa Kairo, na "CAF" ilisisitiza kuwa jambo hilo lilikuwa la kushangaza.


 Na akaunti ya "CAF" kwenye tovuti ya mtandao wa kijamii "Twitter" ilichapisha kipande cha video cha wakati wa wimbo wa kitaifa wa Misri wakati wa moja ya mechi za timu hiyo kwenye mashindano ya mataifa ya Afrika  yaliyofanyika nchini Misri mwaka uliopita.


 Na "CAF" iliandika: "Wimbo wa kitaifa kwa sauti ya watazamaji elfu sabini ... Ni kitu tofauti".


Comments