Al-Khatib atoa bendera na shati ya klabu ya Al-Ahly kwa Mkuu wa Simba ya Tanzania

Mahmoud Al-Khatib Rais wa klabu ya Al-Ahly katika makao makuu ya Al-Jazera (kituo cha Al-Jazera) aliupokea ujumbe wa klabu ya Simba ya Tanzania  uliojumuisha Barbra Gonzalez Mkuu Mtendaji na Malomo Eric Mwanachama wa baraza la idara.


Mahmoud Al-Khatib wakati wa mkutano alijali kukaribisha ujumbe wa Tanzania na kuzungumzia  mahusiano ya kihistoria yanayounganisha klabu ya Al-Ahly pamoja na klabu ya Simba, akisisitiza jukumu la kimsingi la klabu ya Karne katika kuzihudumia klabu za bara na kuhamisha ujuzi wake na katika nyanja zote kusaidia klabu ya Simba katika miradi yake ya baadaye.


 Na Al-Khatib alimpa Mkuu Mtendaji wa klabu ya Simba na Mwanachama wa baraza la idara yake bendera na shati ya Al-Ahly na pia ujumbe wa Tanzania ulimtoa Rais wa Al-Ahly shati ya klabu ya Simba.


Na Al-Khatib alikaribisha kuangalia mpango wa ushirikiano kati ya klabu ya Al-Ahly na Simba ya Tanzania, akisisitiza umuhimu wa jambo hilo kudhamminiwa na Shirikisho la mpira wa miguu la Afrika"CAF". 


Ujumbe wa Tanzania ulionesha hamu yake ya kufaidisha na ujuzi wa klabu ya Al-Ahly katika uwanja wa kimasoko, kiutawala, kimafunzo, vyombo vya habari, na mfumo wa mikataba, hasa baada ya kubadilisha klabu ya Simba kwa kampuni msaada tangu miaka 3 iliyopita.


 Ilikubaliwa Kuwa Simba, klabu ya Tanzania kitatoa wazo kamili la pande za ushirikiano zinazohitajika kati ya klabu mbili katika kipindi kijacho ili kuiangalia kikamilifu. 

Comments