Nour El-Tayeb alitwaa taji la mashindano ya Manchester kwa Boga akimshinda mfaransa Serm

Bingwa wa Misri, Nour El-Tayeb, mchezaji wa Heliopolis na namba nne ya ulimwengu kwa wanawake kwa Boga alishinda mashindano wazi ya Manchester, yaliyoandaliwa na Uingereza kati ya Septemba 16 na 22, na zawadi za kifedha hadi  dola elfu 70, na mashindano hayo yalishuhudia ukuu mkubwa wa kimisri kwa kufikia wawili hao wa Misri kwenye fainali ya wanaume, nao ni Mohammed El-Shorbagy,    akishika nafasi ya kwanza duniani, na Karim Abdel-Gawad, akishika nafasi ya tatu, wakati Nour El-Tayeb akishika nafasi ya nne, alifikia fainali ya wanawake, akikabiliana na mwenye nafasi ya tatu wa Ufaransa Comille Serem.


Nour El-Tayeb alimshinda mshindani wake wa  nafasi ya tatu wa Ufaransa Comille Serem kwa seti tatu kwa moja katika mechi iliyochukua dakika 46, na matokeo ya mechi yalikuwa kama ifuatavyo : 3-11, 11-8, 11-7, 11-3. 


Katika muktadha mwingine, chama cha wachezaji  wataalamu wa Boga "PSA" kilisisitiza umuhimu wa kutumia hatua za tahadhari baada ya kurudi kwa shughuli iliyopangwa kuanza tena katikati ya Septemba katika kupumzika kwa muda mrefu iliyoanza Machi iliyopita kwa sababu ya mlipuko wa Janga jipya la Corona, na  hivi karibuni chama hicho kilitangaza terehe za mashindano 7 yajayo, ambayo ni Manchester, GIB Kimataifa, mashindano ya kimataifa ya Misri huko Pyramids, Hong Kong, El-Gouna International na mashindano ya Black Ball.


Comments