Waziri wa Vijana na Michezo awaheshimu washindi wa " Mpango wa Changamoto ya Vijana 2020"


Dokga Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, aliheshimu timu tano zilizoshinda katika nusu fainali ya Mapango wa " changamoto  ya  vijana 2020," uliozinduliwa na Wizara Januari iliyopita, chini ya kauli mbiu " wakati wetu... jukumu letu... siku zetu za usoni," kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa mataifa kwa Utoto ( UNICEF ), mpango wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa na mpango wa kitaifa wa Plan. 


Sherehe ya heshima, iliyofanyika asubuhi ya leo, Alhamisi katika kituo cha elimu cha kiraia, kwenye Aljazira, ilihudhuriwa na Meja Jenerali Ismail El-Far, mkuu wa idara kuu ya miradi  na idara ya mafunzo ya vijana katika wizara hiyo, Bwana Jeremy Hopkins ni Mhusika wa UNICEF  nchini Misri, Bibi Randa Abu Al-Hassan, mwakilishi mkazi wa mpango wa maendeleo wa Umoja wa mataifa nchini Misri na Bwana Muddathir Siddiqui, Mkurugenzi wa Taasisi ya Plan international Egypt.


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri huyo alieleza kuwa mpango wa " changamoto ya vijana 2020" unaonesha msaada na ulinzi wa uongozi wa kisiasa wa Vijana wa Misri, haswa kwa kuzingatia maeneo ya kufundisha na kuwawezesha  vijana katika kila kitu kinachohusiana na kukuza ubunifu na ujuzi wa ujasiriamali na kuwawezesha ushirikiano kamilifu katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu na kufikia maoni ya Misri 2030, akisisitiza kuwa Wizara inaweka kati ya vipaumbele vyake utekelezaji wa kikundi cha mipango na miradi katika uwanja wa teknolojia, ujasiriamali na stadi za maisha kwa ushirikiano wa taasisi na mashirika ya kimataifa na taasisi zinazohusika na kuwafundisha na kuwawezesha vijana katika mikoa yote ya Misri, kuunda nafasi za ajira kwa vijana na kuwapa ujuzi muhimu ili kuendelea na Soko la ajira na kufikia maendeleo endelevu. 


Sobhy ameongeza kuwa mpango wa changamoto ya vijana wa 2020 unakusudia kuwafundisha vijana ubunifu kwa maendeleo na utekelezaji wa miradi ya ubunifu wa jamii inayotegemea ushirikiano mzuri na inategemea kutoa njia zote endelevu za kupata maisha bora kwa mwanadamu, akitoa wito kwa timu zinazoibuka kufanya bidii zaidi katika ushindani wa kimataifa na kufikia hadhi inayostahili Jamhuri ya Kiarabu ya Misri. 


"Changamoto hii imefikia mwisho wake, lakini ni mwanzo tu wa safari kwa timu hizi tano za wavumbuzi wazuri wa Vijana," alisema Jeremy Hopkins, mwakilishi wa UNICEF huko Misri.  Bwana Hopkins ameongeza, " kupitia hatua kama vile Changamoto ya vijana... Kizazi cha kuanza", na programu ya Mishwary, tutachangia kupeana kizazi kijacho cha vijana wa Misri wanaohitaji kufanikiwa maishani, na pia tunachangia kuwapa nguvu wavulana na wasichana kufikia uwezo wao kamili".


Alimalizia hotuba yake : " ningependa kutoa Shukrani zangu na pongezi kwa Wizara ya vijana na michezo kwa uongozi wake mzuri." Na juu ya kupanua wigo wa mipango yake anuwai ya vijana. Pia, napenda kuwashukuru na kuwapongeza washiriki wetu kwa ushirikiano huo mzuri." 


Kwa upande wake, Bibi Randa Abu Al-Hassan, mwakilishi mkazi wa mpango wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa nchini Misri, alithibitisha kuwa " mpango wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa nchini Misri unaamini uwezo wa Vijana wa Misri nao ni kipaumbele katika shughuli zao mbalimbali kuwapa rasilimali na wanaohitaji kuongoza maisha bora, baadaye na kuwastahilisha kuchukua jukumu kubwa katika kutengeneza kesho inayofaa". Kwa wote, kupitia kufikia malengo ya maendeleo endelevu 2030 na zaidi, matumaini na matarajio. Changamoto ya Vijana 2020 ni moja wapo ya shughuli zimezochangia kuwawezesha vijana ubunifu katika kutatua changamoto za jamii, kuongeza ujasiri na ustadi wao katika kutumikia jamii zao, na kukuza ujasiriamali wa jamii na athari yake kamili na kujenga." 


Pia,  Bibi Randa alimshukuru Dokta Ashraf Sobhy, Waziri huyo, kwa msaada wao wa kudumu na ushirikiano wa manufaa zaidi. 


" Changamoto ya Vijana ilikuwa safari ya kufurahisha iliyojaa  kujifunza, uvumbuzi, ushirikiano na shindano lenye manufaa kati ya vijana, iliyoungwa mkono na ushirikiano thabiti na

Umoja chini ya uongozi wa Wizara ya vijana na michezo", alisema Muddathir Siddiqui, Mkurugenzi wa mpango wa Plan International Egypt.

Na ameongeza:

"Changamoto hii ilithibitisha imani yetu kwamba vijana ndio nguvu ya kuendesha gurudumu la mabadiliko kupitia nguvu zao, shauku na ubunifu, ametoa maoni mengi ya ubunifu wakati wa changamoto hii, ambayo kwa kweli itachangia kupata suluhisho bora kwa maswala ya kijamii mnamo kipindi kijacho".


Mkurugenzi wa Plan International Egypt alithibitisha kuwa :  " katika Plan international, tunafanya kazi katika kuwawezesha na kuwaongoza vijana, na tunazingatia hasa kuwawezesha na kuwaongoza wasichana. Ilikuwa ya kutia moyo sana kwamba karibu  50% ya wanachama wa timu zote zilizoshiriki walikuwa wasichana, na hiyo inatumika kwenye timu tano zilizoshinda, ni muhimu sana kuona wasichana wachanga wakichukua jukumu kubwa katika kukuza jamii zao, pamoja na wenzao wa kiume. 


Shughuli za sherehe hiyo zilijumuisha maonesho ya video ya timu zilizoshinda zilizofikia hatua  inayofuata, nazo ni ( Handy _ Pure _ Gear _ Creative Entity_ Glory ) , na shughuli zimemalizika kwa ufunguzi wa mazungumzo na vijana walioshinda kutoka kwa mipango iliyoshinda, ikifuatiwa na usambazaji wa vyeti kwa washindi. 


Ikumbukwe kuwa mpango huo ulitekelezwa kupitia idara kuu kwa miradi na mafunzo ya vijana katika mikoa 10, nayo ni " Kairo , Aleskandaria , Assiut , Sohag, Qena , Aswan, Kafr El-Sheikh, Beheira, Gharbia, Damietta" , kupitia utekelezaji wa warsha kadhaa za wakufunzi kutoka kwa programu ya Meshwary. Na programu ya uongozi wa vijana, pamoja na utekelezaji kambi 11, na timu tano kutoka kwa mikoa 10 iliyolengwa ziliongezeka, kila timu ilipokea paundi elfu 16 za kubebwa na vyama vilivyoshiriki, kama ufadhilii wa awali, kama kinachofuata, na kuleta athari kubwa katika jamii zao, na timu ( Handy _ Pure kutoka kwa mikoa ya Kairo na Beheira kushiriki katika mashindano ya ulimwengu " changamoto ya vijana" ndani ya mfumo wa mpango wa uzalishaji wa kuanzisha ulimwengu. Timu hizi zitapokea ufadhili wa ziada kwa  Ujasiriamali. 

Comments