waziri awaheshimu vijana wa Wizara wapatao Shahada ya Uzamili MBA kutoka chuo kikuu cha Eslaska cha Ufaransa


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa vijana na michezo aliwaheshimu vijana wa Wizara  waliopata Shahada ya Uzamili katika Idara ya Kazi  kutoka chuo kikuu cha Eslaska cha Ufaransa huko Misri kwa ushirikiano na Wizara ya mipango, ufuatiliaji, na maendeleo ya uchumi, kama sehemu ya kutekeleza mkakati wa maendeleo endelevu (maoni ya Misri 2030) yanayolenga kuongeza ujuzi wa idara wa nchi kupitia kuboresha uwezo wa uongozi, Ustadi wa uongozi  kwa idara ya kati na juu, kila mmoja  katika utaalam wake kwa lengo la kutoa fursa kubwa za kuajiri vijana katika nafasi za uongozi nchini. 


Waziri huyo amesisitiza kwamba Wizara  inatia juhudi kuheshimu vijana vizuri katika jamii katika ngazi zote, na kufanya kazi kupata faida kutoka vijana wenye ujuzi kupitia mpango wa kikamilifu katika maendeleo ya kazi ndani ya Wizara ya vijana na michezo, na kuendeleza kipengele cha kibinadamu kukubaliana na mkakati wa ujenzi wa binadamu uliochukuliwa na uongozi wa kisiasa, na kutunza vizuri kwa vijana katika nyanja zote ili wawe mfano mzuri kwa vijana wengine, na kufanya kazi kuendeleza ujuzi wake,wakiwa viongozi wa kesho katika nyanja zote.


Orodha ilijumuisha majina nane ya vijana waliopata Shahada ya Uzamili kutoka Wizara ya vijana na michezo, nao ni (Dokta Mohammed El-Said Ghonim, Dokta Eman Abd-El gabar Bauomy, Dokta/Ahmad Al-Shafey, Bwana Mohammed Faisel Mohammed, Bwana Ahmad Salah Mostafa, Bibi Wafaa Mohammed Al-Adly, Bwana Hassan Helal Hassan, Bibi Rania Samy).

Comments