Misri yasajili rekodi mpya ya Guinness kwa kubuni neno kubwa zaidi la Amani kwenye kingo za Mfereji wa Suez

Waziri wa Michezo: kuunga mkono kwa uongozi wa kisiasa kwa michezo ya Misri ndio sababu ya mafanikio mapya yote.


Waziri wa Vijana na Michezo Dokta Ashraf Sobhy, alitangaza kuwa Misri imesajili rekodi mpya ya ulimwengu katika Elezo la Guinness, na ilirekodiwa kwa jina la Misri kwa kubuni neno kubwa zaidi la Amani (Peace) na koti 551 za maisha katika muda wa rekodi wa dakika 13 na sekunde 37 kwenye kingo za Mfereji wa Suez, hasa katika  Jiji la Ismailia.


Waziri huyo alieleza kuwa michezo ya Misri inachukua hatua thabiti  na kufikia mafanikio mfululizo kutokana na msaada na uangalizi uliotolewa na Rais Abd El Fatah El-Sisi Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri.


"Sobhy" aliashiria kuwa usajili wa rekodi ya kimisri ulikuja baada ya juhudi kubwa, na kutimizwa kwa mahitaji yote yaliyowekwa na Guinness kwa namba za rekodi kubuni neno kubwa zaidi la Amani,  lililotekelezwa huko Ismailia kwa kuzingatia sherehe za  kimataifa ya Siku ya Amani ya Kimataifa, ili sherehe ya Misri ya Siku ya Amani ya Kimataifa iwe sherehe ya kipekee  ulimwenguni ambao umerekodiwa kwenye Elezo la Rekodi.


Dokta Ashraf Sobhy alishukuru pande zote zinazohusika katika kuandaa tukio hilo ambapo mwanzoni Nahodha Walaa Hafez, Shirikisho la Kuogelea na Uokoaji la kimisri, Mamlaka ya Mfereji wa Suez na vijana wote wa Misri wanaoshiriki katika shughuli hiyo ya ulimwengu.


Namba za Rekodi za Guinness zilikaribisha maombi yaliyohitajika kuwepo zaidi huko Misri, likitaka kusajili rekodi mpya kwake, na Rekodi za Ulimwengu za Guinness ziliahidi kuongeza kuenea kwake huko Misri baada ya utendaji mzuri wa Wamisri katika kufanikisha rekodi katika kubuni neno kubwa zaidi la Amani kwenye kingo za Mfereji wa Suez.

Comments