Mayar Sherif Mmisri wa kwanza aliyefikia ratiba kuu ya mashindano ya Rolan Garos kwa mchezo wa Tenisi

Katika mafanikio ya kipekee katika historia ..
 Mayar Sherif, mchezaji wa timu ya kitaifa ya Tenisi alihakikisha mafanikio ya kipekee ili awe mchezaji Mmisri wa kwanza anayeingia ratiba kuu kwa mojawapo wa mashindano makubwa ya Grand Salam ya Tenisi baada ya kufikia ratiba kuu ya mashindano ya Ufaransa ya kimataifa Rolan Garos mojawapo wa mashindano makubwa na yanayofanyika juu ya Ardhi za mchanga. 


Na bingwa mmisri aliweza kuhakikisha hivyo baada ya kushinda kwake dhidi ya mchezaji wa Italia  Jukia Ghato Montikoni  katika makundi mawili  yalikuwa kama 6-1 /6-3 na kwa hivyo yeye alikuwa mchezaji mmisri wa kwanza aliyefikia mafanikio hayo na mchezaji mwarabu wa pili katika ratiba kuu pamoja na Mtunisia Anas Gaber. 

 

Na Mayar alihakikisha mafanikio hayo baada ya ushindi wake katika mechi tatu miongoni wa  duru zinazofikisha ratiba kuu , ambapo  katika duru ya kwanza alimshinda mchezaji wa Colombia Maria Osoorio 6-4/6-0 kisha katika duru ya pili alimshinda  mchezaji wa Marekani Catherine

Makinly 6-2/6-4 na leo alimshinda mchezaji wa Italia Jukia Ghato Montikoni.Ikumbukwe kuwa Mayar Sherif aliiweka Tiketi yake kwa olimpiki ya Tokyo itakayofanyika Mwaka ujao  baada ya kupata medali ya kidhahabu katika duru ya michezo ya kiafrika


Comments