Waziri wa Michezo afungua uwanja mpya wa Shuti katika kituo cha Olimpiki huko El Maadi

Dokta Ashraf Sobhy : Misri yafanikiwa kuandaa kombe la Dunia la 2021 la Shuti kwenye sahani na kombe la Dunia la 2023 kwa Shuti kwa Bastola na Bunduki.


Leo, Jumatatu, Oktoba 12, Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, amezindua uwanja mpya wa Shuti katika kituo cha Olimpiki huko El Maadi, kwa mahudhurio ya Hazem Hosni, Rais wa mashirikisho ya Misri na Afrika, maafisa wa Olimpiki na mabalozi kadhaa wa nchi za kiarabu, wakiongozwa na Jumaa Mubaraka Al- Junaibi, Balozi wa Emirates nchini Misri na Bassam Darwish, Balozi wa Syria nchini Misri, pamoja na marais wengine wa bodi za wakurugenzi za vilabu vya Shuti na japo la viongozi wa Wizara.


Waziri huyo alisema kuwa ufunguzi wa uwanja mpya wa Shuti unaojumuisha uwanja wa shinikizo la hewa wa mita 10 iliyogawanywa na vichochoro  18 na huweza kupokea idadi kubwa zaidi ya mashindano iwe ya ndani au kiwango cha kimataifa, ni uwanja wa kuanza wa kufundisha timu za Shirikisho la Shuti la Misri kujiandaa na Olimpiki ya Tokyo 2021,  nao ni mafanikio kwa Shirikisho, kwa kuzingatia kujali kunachoshikiliwa na serikali kwenye mchezo wa Shuti na kuhangaika kila wakati kushinda vizuizi vyote vinavyokabili mchezo huo.


Dokta Ashraf Sobhy alisema kuwa : " Miongoni mwa mafanikio ya nchi katika kuandaa matukio, hafla kuu na imani ya ulimwengu huko nje na mashindano yote ya kimataifa kwa njia bora, tulifanikiwa kwa shukrani za mshikamano na ushirikiano wa kila mtu katika faili la kuandaa kombe la Dunia la Shuti ( Risasi ) kutoka Februari 26 hadi Machi 8, 2021 na kombe la Dunia la Shuti na vijana wa Bastola na Bunduki, iliyopangwa 2023 katika moja ya matukio muhimu zaidi katika  mchezo huo".


Hazem Hosni, Rais wa mashirikisho mawili ya mchezo wa Shuti ya Misri na Afrika, alionesha mafanikio ya shirikisho na timu yaliyohakikishwa wakati wa mwisho na msaada wa Wizara ya vijana na michezo ikiongozwa na Dokta Ashraf Sobhy, Waziri ya Ulinzi na Mambo ya Ndani na Kamati ya Olimpiki.


Alimshukuru Waziri wa Vijana na Michezo, Kamati ya Olimpiki na Waziri ya Ulinzi na Mambo ya Ndani kwa msaada wao wa kila wakati unaosaidia   Shirikisho la Shuti kufanikisha yote yanayofanyika kwenye nchini Misri, akisisitiza kuwa uwanja huo ni sehemu ya mpango wa Shirikisho kupanua mazoezi ya michezo kote Jamhuri ili kusambaza timu za kitaifa kwa vipaji.


Pia, Waziri wa Michezo alikagua mazoezi ya timu ya Misri kwa kujiandaa na mashindano ya Karate ya Dunia.


Kwa kumalizia, Waziri huyo aliwaheshimu wafanyakazi na wale wanaowajibika kuandaa uwanja mpya wa Shuti kwa kutoa vyeti vya shukrani kutathmini juhudi zao.

Comments