Waziri wa Michezo ashuhudia sherehe za wachanga wa mradi wa kitaifa wa Boga


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alishuhudia maadhimisho ya mradi wa kitaifa wa vipaji vya Boga kwenye Siku ya Boga Duniani kwenye klabu ya El Nady, huko mji wa 6 Oktoba  kwa mahudhurio ya Asim Khalifa, Rais wa Shirikisho la Boga la Misri, Amir Wajih, mshauri wa kiufundi wa mradi huo, Mohamed Hamdy, Mkurugenzi Mkuu wa Vipaji vya Michezo, na Bodi ya Wadhamini wa Klabu ya El Nady.


Wakati wa hafla hiyo, Waziri huyo, Dokta Ashraf Sobhy alisifu kiwango cha ufundi cha Wachezaji wa kiume  na wa kike wa mradi huo, akielekeza umuhimu wa kufuata viwango na vipimo vyote vya kimataifa katika mafunzo, na kusajili wachezaji wa mradi katika Shirikisho la Boga la Misri.


Waziri huyo alisisitiza kuwa mradi unakusudia, ndani ya miaka 5, kutoa wataalam mashuhuri kwa timu za Boga za Misri, kudumisha nafasi na msimamo wa uongozi wa Boga kwa Misri  ulimwenguni.


Wizara ya Vijana na Michezo ilizindua vipimo vya uteuzi wa Mradi wa Kitaifa wa Vipaji vya Boga chini ya usimamizi wa Benki ya Kitaifa kama sehemu ya Mradi wa Kitaifa wa Zawadi na Bingwa wa Olimpiki mnamo Januari jana kuchagua wanariadha 250 bora zaidi kutoka kwa waombaji katika mkoa wa Kairo na Port Said.Waombaji walipimwa na kuchaguliwa na wataalam wakuu katika uwanja wa Boga kwa kushirikiana na  Shirikisho la Boga la Misri, wana wa mashahidi wa vikosi vya jeshi, polisi na yatima wanawakilisha  20% ya  washiriki.Huu ni uthibitisho kwamba serikali ya Misri haiwasahau wanawe  waliotoa maisha yao kwa ajili ya nchi yao.


Ikumbukwe kwamba washiriki wa mradi huo ni kati ya talanta zinazoibuka ambao walizaliwa mnamo 2012, 2013 na 2014 katika mchezo wa Boga.  Kuunda msingi mpana wa watendaji wa Boga, na kuandaa vizazi vipya vya mchezo huo.


Katika muktadha huo huo, Waziri wa Michezo alifanya ziara ya ukaguzi wa klabu ya El Nady, ambayo ni pamoja na vyumba vya kubadilishia nguo, viwanja vya Tenisi ya ardhini, ukumbi wa michezo wa Kirumi, Idara ya mahusiano ya Umma, na wakati wa ziara hiyo alisikiliza  ufafanuzi kutoka kwa Bodi ya Wadhamini wa klabu juu ya vifaa na huduma muhimu zaidi kuongezwa wakati wa awamu ifuatayo.

Comments