Mohamed El Shenawy aongoza orodha ya magolikipa 5 bora zaidi barani Afrika


Ukurasa  rasmi wa Intaneti wa Shirikisho la kimataifa la Soka “FIFA” kwenye Twitter ulitoa ripoti iliyojumuisha magolikipa 5 bora zaidi barani Afrika sasa hivi, pamoja na kukaribia kuanza kwa Fainali za kiafrika zinazofikisha mashindano ya kombe la Dunia 2022, na Mohamed El Shenawy -Golikipa wa timu ya nchi Misri na klabu ya Al Ahly- aliongoza orodha ya magolikipa 5 bora zaidi barani Afrika sasa hivi.


Mmorocco Yassien Bono –Golikipa wa klabu wa Uhispania Sevilla-, Msengal Edward Mendi –Golikipa wa klabu ya Uingereza Chelsea-, na Mcameron Andreh Onana –Golikipa wa klabu ya Uholanzi Ajax Amsterdam- wapo katika orodha ya magolikipa bora zaidi barani Afrika, pamoja na Mohamed El Shenawy.


“FIFA” imesema juu ya Mohamed Al Shenawi: “njia ya mmisri Mohamed El Shenawy haikuwa rahisi kamwe , na lazima kukumbusha kuwa Golikipa wa awali katika timu ya nchi yake alikuwa Issam Al Hadari, hadithi ya mpira wa kiafrika wa miguu aliyekuwa alilinda pango la mafarao hadi umri  wa 45, kwa hivyo amekuwa –katika mashindano ya Urusi 2018-  mchezaji mkubwa zaidi anayeshiriki katika Fainali za kombe la Dunia, lakini pamoja na hivyo AL Shenawi hakusimama bila kufanya chochote, na alijitahidi kwa jukumu kubwa na klabu yake Al Ahly mnamo mwaka 2016. Wakati ambapo  Kiongozi wa mashetani wekundu alishinda matoleo matutu ya mwisho kutoka ligi ya kitaifa, na alifikia kwa ubora na kwa mraba wa dhahabu katika ligi ya mabingwa wa Afrika.


Iliendelea: “na kwenye kiwango cha timu za nchi, alicheza kama mchezaji mkuu katika mashindano ya kwanza ya timu ya nchi yake huko Urusi mwaka 2018, amechaguliwa kama mtu wa mashindano dhidi ya Uruguay (1-0), na katika kilele cha kiwango chake mnamo miaka ya 31, Al Shenawi anatarajia kuongoza Misri kwa Fainali za kombe la Dunia kwa mara ya pili mfululizo, ambapo kura imeiweka Misri kando ya Gabon, Libya, na Angola.

Comments