Waziri wa michezo ashuhudia tamasha la michezo huko Bashayer na Mfereji wa Mahmoudia mjini Aleskandaria

 Ijumaa Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa vijana na michezo anashuhudia tamasha la michezo kwa wanawake    linaloandaliwa na idara kuu ya maendeleo ya michezo ,Kwa kushirikiana na baraza la kitaifa la wanawake , kurugenzi la vijana na michezo  mkoani mwa Aleskandaria na kamati ya wanawake  ya olimpiki ya Misri nalo, linajumuisha  " mashindano ya mbio za Baiskeli  kuanzia mbele ya mfereji wa  Mahamudia hadi El-bashayer ,mbio ya kutembea kwa wanawake ndani ya viwanja vya Bashayer El-kher , mechi ya mpira wa wavu , mechi ya Fainali ya mpira wa Tenisi ya meza , mechi ya pande tano za mpira wa miguu , mpira wa kasi na mashindano ya mazoezi ya misuli " vilevile , tamasha linajumuisha mchezo wa  kuigiza wa unyanyasaji dhidi ya wanawake .


Hii inakuja katika mfumo wa maadhimisho ya kumbukumbu ya  miaka 47 ushindi wa vita vya Oktoba   na kusisitizia  jukumu la kijamii la Wizara na mchango wake katika kutangaza miradi ya kitaifa na utiliaji mkazo wa Wizara kwa jukumu la mwanamke na kuongeza shughuli zinazohusiana msichana na mwanamke.


 Kwa upande mwingine  , Dokta Ashaf Sobhy, Waziri huyo alitembelea akikagua  kurugenzi la vijana na michezo,ambapo  alifungua  ukumbi wa mazoezi ya misuli " GM"  , Dimbwi la kuogelea na uwanja wa pande tano katika kituo cha vijana wa Abes.

Comments