Uchaguzi wa mchezaji wa Taikondo wa Misri Abeer Essawy kuwa Mwanachama katika Ofisi ya kiutendaji ya Wanariadha wa Olimpiki

Abeer Essawy , mwanariadha wa Olimpiki wa Taikondo, alichaguliwa kwa Ofisi ya Utendaji ya Wanariadha wa Olimpiki "WOA" kama mwakilishi wa Afrika.


Abeer alichaguliwa kati ya wanachama wengine wapya, wakati alichaguliwa tena Rais wa Ofisi ya Utendaji ya Wanariadha wa Olimpiki Duniani WOA na wanachama tisa.


Abeer Essawy ni bingwa wa Taikondo na alishiriki kwenye Michezo ya Olimpiki huko Athene mnamo 2004, wakati alikuwa na umri wa miaka kumi na saba, alishinda mashindano mengi ya taifa na ya kimataifa, na akashinda Ubingwa wa Afrika kwa miaka mitano mfululizo kutoka 2003 hadi 2007.


Comments