Waziri Mkuu akagua shughuli za ukumbi uliofunikwa mjini 6 Oktoba kujiandaa kwa Kombe la Dunia la Mikono


 Dakta Mostafa Madbouly, Waziri Mkuu, alikagua kumaliza kwa ukumbi uliofunikwa mjini 6 Oktoba, utakaokuwa kati ya viwanja vitakavyoshiriki shughuli za Mashindano ya Mpira wa Mikono Ulimwenguni ya 2021, ambayo ni pamoja na makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa mikono la Misri na Chuo cha Mpira wa mikono cha Afrika, akifuatana na Dokta Ashraf Sobhy,  Waziri wa Vijana na Michezo, Dokta Asim Al-Jazzar, Waziri wa Nyumba, Huduma na Jamii za Mjini, na Dokta Hassan Mustafa, Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa mikono.


 Wakati wa ziara yake, Waziri Mkuu alisikiliza maelezo kamili ya kile ambacho kimekamilika kwa kazi inayoendelea hivi sasa, kwani kiwango cha utekelezaji kilifikia 95%, Dokta Moustafa Madbouly aliagiza kukamilika kwa haraka kwa kazi zote kulingana na muda uliowekwa. 


 Waziri Mkuu ameongeza kuwa Misri kwa sasa inakabiliwa na kasi kubwa ya michezo, iwe kwa mafanikio, idadi na mashindano, au vituo vya michezo, akisisitiza utekelezaji wa maagizo ya uongozi wa kisiasa katika suala hilo.


 Waziri wa Vijana na Michezo alionesha kuwa ukumbi wa mazoezi uliofunikwa,  unaoweza kuchukua watazamaji 4,500, itakuwa nyongeza kwa miundombinu ya michezo, pia ni moja ya kumbi bora zaidi katika Mashariki ya Kati ambayo ilianzishwa kulingana na udhibiti na viwango vilivyowekwa na Shirikisho la Kimataifa la Mchezo.

Comments