Wizara ya vijana na michezo yapanga ziara ya kiutalii kwa ujumbe wa timu ya taifa ya Brazil ya kiolimpiki


Idara ya utalii wa kimchezo ilipanga ziara ya kiutalii ,pamoja na Wizara ya vijana na michezo na kwa ushirikiano na wizara ya Utalii na mabaki ya kale ,kwa ujumbe wa timu ya taifa ya Brazil ya kiolimpiki pembezoni mwa ushiriki wao kwa kipindi cha kiolimpiki ya kimataifa kilichofanyika nchini Misri . 


Ziara hiyo ilijumuisha kutembelea makumbusho ya  Kimisri na Piramidi pamoja na waongozo wa watalii , walioelezea historia ya uanzishaji wa Piramidi na Sphinx  , na vipengele vya makumbusho ya Kimisri na mabaki ya kale linayo , na enzi za mabaki hayo . 


Wanachama wa ujumbe huo walieleza furaha yao kwa ustaarabu wa Misri , na historia na mabaki ya kale yaliyopo nchini Misri , wakisifu namna walivyopokelewa na mahali walipopaishi mjini Kairo . 


Timu ya taifa ya  Brazil ya kiolimpiki ilishiriki kwenye mashindano ya kipindi cha urafiki cha kiolimpiki pamoja na timu ya Misri na ya Korea kusini  , iliyomalizika na ushindi wa timu ya kimisri ya kiolimpiki kwa nukta 4 baada ya kupata sare pamoja na timu ya Korea kusini na kushinda timu ya Brazil .

Comments