Waziri wa michezo apokea ujumbe wa timu ya kitaifa katika uwanja wa ndege wa Kairo


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa vijana na michezo amepokea ujumbe wa timu ya kitaifa ya Misri ya mpira wa miguu baada ya kurejea kwao kutoka Togo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kairo na hivyo baada ya kushinda kwao dhidi ya timu ya kitaifa ya Togo katika Mashindano ya Mataifa Ya Afrika 2021 huko Cameron. 


Na wakati wa mkutano wake na wachezaji wa timu ya kitaifa , Dokta Ashraf Sobhy aliwaeleza furaha na shukurani kwa wachezaji na Wafanyikazi wa kiufundi na kiutawala wa timu ya kitaifa kwa juhudi na utendaji wao wa kipekee 

Na kuishinda  Togo nje ya nchi ili wawe karibu na ustahili wa kawaida wa timu ya kitaifa kwa mashindano ya Afrika.


Na Waziri aliwaomba kufanya juhudi za ziada kupitia mechi zijazo ili kufurahisha mashabiki wa mpira wa miguu wa Misri kupitia matokeo ya kufurahisha na utendaji bora , akiashiria kwamba mpira wa miguu wa Misri unashuhudia maendeleo kuhusu timu ya kitaifa ya kwanza , Timu ya kitaifa ya kiolimpiki na timu ya kitaifa ya vijana pamoja na viwanja vya klabu ambazo zikawa zinaongoza eneo la mpira wa miguu katika barani Afrika.


Na Dokta Ashraf Sobhy, Waziri huyo alihudhuria mechi ya timu ya kitaifa ya kiolimpiki na timu ya kitaifa ya Brazil iliyofanyika katika uwanja wa Kairo usiku wa jana katika duru ya kirafiki ya kimataifa ambapo Misri , Brazil na Korea kusini zinashiriki kwenyewe na inayozingatiwa kujiandaa kwa kushiriki katika olimpiki ya Tokyo 2021 na timu ya kitaifa ya Misri imeweza kuishinda  timu ya kitaifa ya Brazil katika mechi kati ya timu hizo mbili kwa matokeo ya mabao mawili dhidi ya bao moja.

Comments