Waziri wa vijana akagua mji wa kimichezo na ukumbi unaofunikwa huko mji mkuu wa kiutawala


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa vijana na michezo alikuwa akikagua mji wa kimichezo huko mji mkuu mpya wa kiutawala ; ili kuainisha kiwango cha mafanikio yaliyofikiwa kwa upande wa miundombinu katika mji wenye ukubwa wa eneo la ekari 93 , na hivyo kwa kusindikiza maafisa wa idara ya kazi za kijeshi kwenye taasisi ya uhandisi kwa vikosi vya kijeshi wanaohusika  kazi za utekelezaji . 


Ziara hiyo ya Waziri ya kukagua ilijumuisha  mkusanyiko wa viwanja ,  eneo la michezo ya pamoja , viwanja vya shughuli mbalimbali , mahali pahusika kwa  familia na watoto , kumbi za michezo za umoja , mkusanyiko wa mabwawa ya kuogelea , viwanja vya tenisi , jengo la uwanja wa Boga, jengo la utamaduni la kiteknolojia , jengo la kijamii , eneo la huduma  , pamoja na kukagua ukumbi unaofunikwa  ambao umeshafanyiwa na imepangwa ukaribishwe  mojawapo ya makundi ya michuano ya dunia ya mpira wa mikono itakayokaribishwa na Misri mnamo Januari ijayo .


Dokta Ashraf Sobhy   alifafanua kwamba mji wa kimichezo unazingatiwa kuwa mojawapo ya viwanja vikubwa  zaidi vya michezo nchni Misri  vilivyofanywa kutokana na vigezo vya kimataifa , na vinazingatiwa kuwa mafanikio mapya kwa majengo ya kimichezo yanayotofautisha Misri na yanayosambaa kwenye pembe zote za Jamhuri , akiashiria kuwa mji huo ni mojawapo ya miradi ya ajabu  huko mji mkuu mpya wa kiutawala ambao miongoni mwa miradi ya kitaifa inayokuwepo nchini Misri mnamo uongozi wa Rais Abd El-Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri . 


Waziri huyo alisifu kiwango cha mafanikio yaliyokamilishwa  kwa upande wa miundombinu katika mji wa kimichezo huko mji mkuu mpya wa kiutawala na vilevile imeshamalizika kufanya ukumbi unaofunikwa ndani ya mji , na kujiandaa ili kukaribisha mashindano ya michuano ya dunia kwa mpira wa mikono 2021 , akiashiria utiliaji maanani  wa Misri ; kufikia mafanikio katika kuandaa kombe la dunia  la mpira wa mikono na wote wanatilia mkazo kushikamana kwa ajili kutoa michuano katika sura bora  zaidi inayoonesha Ulimwenguni kote uwezo wa Misri wa kupokea  michuano mikubwa zaidi ya kimichezo ya kimataifa.

Comments