Mawaziri wa Vijana, Uzalishaji, Elimu na Umwagiliaji wazindua Ligi ya Wizara


Waziri wa Vijana na Michezo Dokta  Ashraf Sobhy, Waziri wa Elimu ya Juu na Utafiti wa Sayansi Dokta Khaled Abd El Ghaffar, Meja Jenerali Mhandisi Mohamed Ahmed Morsi, Waziri wa Nchi kwa Uzalishaji wa Jeshi na Dokta Mohamed Abd El Aty Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji walishuhudia Kufunguliwa kwa mashindano ya kwanza ya Wizara ya  Khomasi ya mpira wa miguu ya wanaume na tenisi ya meza kwa wanawake kwenye Kituo cha Olimpiki huko Maadi, kwa mahudhurio ya wawakilishi wa wizara zinazoshiriki na mashirikisho mbalimbali ya michezo na kikundi cha wachezaji wa mpira wa miguu na michezo ya misri chini ya kaulimbiu "Misri ipo kwanza .. La kwa Msimamo mkali"


Katika hotuba yake Waziri wa Vijana Dokta Ashraf Sobhy alielezea furaha yake kubwa wakati wa ufunguzi wa ligi ya kwanza ya wizara, akitamani kuwa ungekuwa mwanzo wa mfululizo wa vikao vya michezo vinavyolenga ushiriki wa jamii ya washiriki wa vifaa vya serikali, pamoja na kuchochea kufanya mchezo kuwa njia ya maisha, kulingana na mpango "Misri ipo Kwanza .. La kwa Msimamo mkali. "


Waziri wa Vijana na Michezo Dokta Ashraf Sobhy alithibitisha kuwa wazo la ligi hiyo lilitokana na utiliaji muhimu wa Mheshimiwa Abd El Fatah El-Sisi Rais wa Jamhuri kwa afya ya raia na kuwahamasisha kufanya mazoezi ya michezo kila siku, chini ya uangalifu mkubwa wa Mheshimiwa Waziri Mkuu Mustafa Madbouly.


Mashindano hayo yatafanyika kutoka 21 hadi 30 mwezi wa Novemba chini ya kauli mbiu "Michezo kwa Burudani na Maisha" iliyoandaliwa na Idara kuu kwa Maendeleo ya Michezo kwenye Wizara ya Vijana na Michezo na Shirikisho la umma la Michezo kwa Wafanyikazi wa Serikali katika michezo miwili ya Khomasi ya mpira wa miguu wa wanaume na tenisi ya meza ya wanawake na ushiriki wa washiriki 510 na ushiriki wa wizara 23 na Diwani kuu ya Baraza Kuu la Mawaziri na washiriki 15 kutoka kila wizara.


 Kura hiyo ilifanywa na ushiriki wa kikundi cha wachezaji wa michezo wa Misri Abd El Hamid Bassiouni, Islam Al-Shater, Wael Riad, Metamed Gamal, kocha Shawky Gharib mkurugenzi wa kiufundi wa timu ya Olimpiki, Mutasim Salem na Osama Abd El Karim na Marefa Amin Amr, Samir Othman na Ayman Djesh.


Bahati nasibu hiyo ilisababisha Wizara ya Vijana na Michezo kuwepo katika kundi la pili pamoja na Wizara za Ugavi, Upangaji, Nguvu kazi, Utalii na Mambo ya nje na katika kundi la kwanza hupatikana wizara  za Kilimo na Ushirikiano wa Kimataifa, Diwani ya Ofisi ya Baraza la Mawaziri, Maendeleo ya Mitaa, El Awkaf na Mawasiliano.


Katika kundi la tatu zilikuja wizara za mabunge, biashara, viwanda, elimu ya juu, afya, uchukuzi na fedha, wakati kundi la nne na la mwisho lilitoka kwa wizara za utamaduni, Sekta ya Ujasiriamali, nyumba, uzalishaji wa kijeshi, elimu, na mambo ya nje.


Wakati wa sherehe ya ufunguzi, kikundi cha maonyesho ya muziki na sauti kilifanywa na mwimbaji Ahmed Gamal.


Na pembezoni mwa sherehe; Mechi ya maonyesho ilifanyika kati ya Waziri wa Vijana na Michezo ,  Waziri wa Elimu ya Juu na wachezaji wakubwa wa mpira wa miguu waliohudhuria sherehe hiyo

Comments