Waziri wa michezo :Uimarishaji wote kwa Karim Darwish kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Boga la Kimataifa


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa vijana na michezo alisisitiza kutoa msaada wowote , kwa bingwa wa dunia Karim Darwish kwenye uchaguzi wa cheo cha Naibu Rais wa Shirikisho la Boga la Kimataifa , ili kuwakilisha Misri kwenye kiwango cha kimataifa katika mchezo huo ambao wachezaji wa Misri wanautawala kwenye mashindano ya wanawake na wanaume .


Hiyo ilikuwa kupitia mkutano wa waziri wa vijana na michezo pamoja na Asem Khalifa Mkuu wa Shirikisho la Boga la kimisri , na Karim Darwish bingwa wa dunia wa zamani kwenye mchezo wa Boga ; ili kuonesha maandalizi ya mchezaji kuanza uchaguzi wa Shirikisho la Boga la Kimataifa kwa cheo cha naibu Rais , ambao utafanyika Desemba ijayo .


Dokta Ashraf Sobhy akatamani ushindi kwa bingwa wa Misri Karim Darwish kwenye uchaguzi huo , akisifu uzoefu wake wa uongozi na uwezo wake wa kushindana kwenye uchaguzi na kushinda .


Mkutano ulizungumzia maandalizi ya Shirikisho la Boga la kimisri  kwa ubingwa ujao wa kimataifa  , na mipango ya kimafunzo inayohusu wachezaji , vilevile maonesho ya maono ya wizara kwa ushikamano na Shirikisho katika kupanuka kwa uenezaji wa mchezo wa Boga kwenye kiwango cha mikoa yote , na kukagua  wenye vipaji  kwenye mfumo wa kuhifadhi uongozi wa Misri duniani katika mchezo huo.

Comments