Waziri wa michezo : kuhudhuria kwa Rais sherehe ya ufunguzi wa kombe la dunia kuashiria ufadhili usio na mipaka kwa michuano


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa vijana na michezo alisifu sherehe ya ufunguzi wa mashindano ya ulimwengu kwa mpira wa mikono yanayopokelewa kwa Misri mnamo kipindi cha 13 mpaka 31 Januari, iliyofanyika kwenye uwanja wa Kairo kwa  kuhudhuria kwa Rais wa Jamhuri Abd El-Fatah El Sisi.


Sobhy ameshasema kwamba sherehe ilipangwa vizuri na kusifiwa na jumbe zote zilizoshiriki katika kombe la Dunia , zilizoelezea  furaha yake kwa utaratibu mzuri .

 

Akiongeza kwamba kuhudhuria kwa  Mheshimiwa Rais Abd El-Fatah El Sisi huongeza uzuri wa sherehe, linalosisitiza ufadhili na msaada wa nchi ya Misri na uongozi wa kisiasa kwa mashindano ya ulimwengu wa mpira wa mikono, haswa kufanyika kwake ndani ya mazingira maalumu wakati wa usambazaji wa virusi vya Corona, katika wimbi lake la pili, ambalo ni ujumbe kwa watu wote duniani kwamba Misri inaweza kupanga michuano, na iko tayari kwa majukumu ya viwango vyote.

Comments