Waziri wa Michezo asifu utendaji wa kishujaa kwa timu ya taifa licha ya kushindwa kutoka kwa timu ya taifa ya Uswidi na Sanad ni mtu wa mechi


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alisifu utendaji wa wachezaji wa timu ya taifa ya Misri licha ya kushindwa kutoka kwa Uswidi kwa matokeo 24-23, mwishoni mwa mechi za kundi  la saba, ndani ya mashindano ya michuano ya mpira wa mikono ulimwenguni, yanayokaribishwa huko Misri hadi Januari 31 kwa ushiriki wa timu 32.


Mechi hiyo ilihudhuriwa na Dokta Hassan Mostafa, Rais wa Shirikisho la kimataifa la Mpira wa Mikono, Bwana Per Axel Frillinsdorf, Balozi wa Uswidi nchini Misri na Mhandisi Hisham Hatab, Rais wa kamati ya Olimpiki ya kimisri.


Na matokeo ya kipindi cha kwanza yalimalizika kwa kiwango cha juu cha kimisri kwa matokeo 12-9 na timu hizo mbili zilibadilishana udhabiti wa mwenendo wa mechi, timu ya Misri ilibaki mbele wakati wote wa mechi hadi timu ya kitaifa ya Uswidi iliweza kurekebisha matokeo na kuiteka mechi hiyo kwa sekunde za mwisho kwa matokeo ya 24-23, hivyo kufikia timu ya Misri kwa jukumu kuu kama namba mbili ndani ya kundi la saba iko nyuma Kiongozi wa kundi "Uswidi" na timu ya Makedonia iko katika nafasi ya tatu, iliyoweza kuishinda timu ya kitaifa Chile kwa matokeo 32-29 katika mechi kati ya Misri na Uswidi na timu ya Chile ilihamia kucheza kwenye mechi za " Kombe la Rais ", baada ya kushindwa kupata alama yoyote katika kikundi hicho, timu tatu hizo zitajiunga kwa Urusi ,Belarusi na Slivenia katika kundi moja.


Waziri wa Vijana na Michezo alitoa ombi kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Mafarao kujitahidi zaidi kuwafurahisha mashabiki wa Misri kutwaa taji la ubingwa, kupanda jukwaani na kipanda kiti cha enzi cha mpira wa mikono duniani.


Timu ya mpira wa mikono ya Misri ilicheza mech hii kwa orodha hiyo ya makabiliano ya mwisho ya Mekedonia, yaliyosababisha  kuingiza Ahmed Al-Ahmar  badala ya Mohsen Ramadan.


Orodha ya wachezaji ya mechi inaojumuisha: Karim Hindawi - Mohammed Essam Al-Tayyar - Omar Al-Wakeel - Ahmed Moamen - Ali Zain - Yahya Al-Daraa - Hassan Qaddah - Ahmed Hisham Al-Sayad - Saif Al-Daraa - Yahya Khaled - Ahmed Al-Ahmar - Mohammed Sanad - Akram Yousry  Mohammed Mamdouh Hashem - Ibrahim Al-Masry - Wissam Nawar.


Inapaswa kuashiria kwamba kombe la mikono la Dunia katika toleo lake la 27 linahudhuriwa kwa timu 32 kutoka nchi tofauti za ulimwengu kwa mara ya kwanza na Misri itaikaribisha mnamo Januari 13-31, 2021 kwa kutumia mfumo wa Bubble ya matibabu kwa timu zote na wanachama wa ujumbe wanaoshiriki kwenye mashindano hayo.


Mashindano hayo yanafanyika katika kumbi 4 nazo ni : ukumbi mkuu wa uwanja wa Kairo, ukumbi wa mji mkuu wa kiutawala,  ukumbi wa Borg Al-Arab na ukumbi wa Dokta Hassan Mostafa mjini 6 Oktoba.

Comments