Hisham Nasr akutana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Mikono Afrika na wakuu wa jumbe za timu


Jumapili, Mhandisi Hisham Nasr, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Mikono la Misri, alikutana na Mansour Arimou, Rais wa Shirikisho la Afrika na wakuu wa timu za kitaifa katika kikundi  cha mji mkuu wa kiutawala kinachoshiriki mashindano ya Dunia kwenye toleo lake la 27 kwa mpira wa mikono kwa wanaume, yanayokaribishwa kwa Misri kuanzia Januari 13 hadi 31.


Mkutano huo ulikuwa pamoja na kubadilishana maneno ya kukaribishwa na kusifiwa kutoka kwa wakuu wa ujumbe, Mansour Arimou, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Mikono Afrika, Habib Laban, Mkuu wa ujumbe wa timu ya kitaifa ya Algeria na Mkuu wa Shirikisho la mpira wa mikono la Algeria, Adli Al Hanafi, Mkuu wa ujumbe wa timu ya kitaifa ya Morocco, Rais wa chuo kikuu cha kifalme cha Morocco cha mpira wa mikono na Moaz bin Zan Zayed Mkuu wa ujumbe wa timu ya kitaifa ya Tunisia.


Mkutano huo ulishughulikia kutoa Shukrani kwa serikali na watu wa Misri kwa upangaji mzuri wa mashindano ya Dunia, kwani Misri iliweza kufanya mashindano hayo wakati wa hali ngumu unaoenea Duniani, na licha ya hayo, kwa kuchukua hatua zote za tahadhari, mashindano yalifanyikwa mnamo wakati wake maalum.


Waheshimiwa Wakuu wa jumbe walithibitisha kuwa makao makuu ya timu katika mji mkuu wa kiutawala yako katika kiwango cha juu na ukumbi uliofunikwa ambao mechi hufanyika katika mji mkuu wa kiutawala bila shaka ni kito cha michezo na kuna msisitizo mkubwa juu ya kuchukua hatua zote za tahadhari na kufanya upimaji kwa timu zote kila masaa 24 mfululizo kuangalia afya ya wajumbe wote na kamati iandaayo.


Mhandisi Hisham Nasr alikutana na kamati ziandaazo  mashindano hayo na Shirikisho la kimataifa la mpira wa mikono  na kusikiliza sifa na furaha yao kwa kufanya mashindano mnamo wakati wake maalum na mipango mizuri  ya nchi ya Misri kwenye mashindano ya Dunia.


Ziara ya Mhandisi Hisham Nasr, Rais wa Shirikisho la Misri la Mpira wa Mikono kwenye makao makuu ya jumbe za timu zinazoshiriki mashindano ya Dunia inakuja pamoja na kuchukua hatua zote za tahadhari wakati wa kuwepo wote ndani  ya Bubble iliyofungwa ya mashindano.

Comments