Mkuu wa Shirikisho la kimataifa la mpira wa mikono amshukuru Waziri wa michezoDokta " Hassan Mostfa " Mkuu wa Shirikisho la kimataifa la mpira wa mikono alipeleka ujumbe wa Shukrani kwa Mheshimiwa Dokta "Ashraf Sobhy"  Waziri wa vijana na michezo , Dokta.Hala Zaied "Waziri wa Afya na Wakazi", Dokta "Alaa Eid "Mkuu wa kundi la matibabu kwenye Wizara ya Afya na Wakazi na Mkuu wa kamati ya matibabu kwa michuano  kwa  kushirikisha kwao katika mkutano wa wakuu wa wajumbe wanaoshiriki na kuhakikisha taratibu za kiafya za dharura ili kuwalinda   waoshiriki katika kombe la Dunia . 


 Bwana.Mostafa alielezea Shukrani zake kamili  kwa mawaziri wawili wa michezo na  Afya kwa ajili ya kutilia maanani mara kwa mara kwa shughuli zote za kombe la dunia  pamoja na kusisitizia daima umuhimu wa  kufuatilia hatua zote za tahadhari   na hatua za kujizuia , akipa uthamini wake mkubwa  kwa juhudi kubwa zinazotekelezwa ili kuhakikisha maandalizi mazuri kwa  michuano ya dunia ya wanaume 2021 . 


 Ikumbukwe kuwa Mheshimiwa Dokta " Ashraf Sobhy " Waziri wa vijana na michezo na Dokta " Hala Zaied " Waziri wa Afya na Wakazi,leo  asubuhi, walifanya mkutano pamoja na wakuu wa wajumbe wanaoshiriki kwenye michuano ya dunia ya mpira wa mikono  na hayo kupitia mbinu wa video Conference  kwa lengo la kutilia mkazo kwao kwa taratibu za dharura ili kuwalinda waoshiriki katika kombe la dunia . 


Mkutano huo ulihudhuriwa na Dokta " Hassan Mostfa " Mkuu wa Shirikisho la kimataifa la mpira wa mikono, Kocha" Hassan  Labib " Mkuu wa toleo la 27 la michuano ya dunia kwa mpira wa mikono wa  wanaume na Dokta " Alaa Eid " Mkuu wa kamati ya matibabu ya michuano .

Comments