Waziri wa Michezo na Mwenyekiti wa Shirikisho la Kimataifa la mpira wa mikono washuhudia mechi ya Angola na Japan katika ukumbi uliofunikwa huko Aleskandaria


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, na Dokta Hassan Mustafa, Mwenyekiti wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa mikono, wanashuhudia mechi kati ya timu za Japan na Angola miongoni mwa  mashindano ya kundi la tatu la Mashindano ya Mpira wa Mikono  Duniani 2021 huko Misri, kwa mahudhurio ya wawakilishi kadhaa wa Ubalozi wa Angola, na kocha Mahmoud Al-Khatib, Rais wa Klabu ya Al-Ahly.


Waziri huyo alihakikishia vifaa na hatua zote zilizochukuliwa katika ukumbi uliofunikwa kwenye Borg Al Arab huko Aleskandaria kabla ya kuanza kwa mchezo huo, kwani ukumbi huo unashiriki mashindano ya kundi la tatu na la nane, na Waziri pia aliangalia kufuatilia kwa waandaaji wote wa ukumbi kwa hatua zote na tahadhari za kuzuia virusi vya Corona.


Kundi la tatu lajumuisha timu za Croatia, Qatar, Japan na Angola, na timu ya Qatar imehakikishia kufikia duru  ya pili katika raundi ya pili baada ya kuishinda Japan na kupata alama 4 za kufikia raundi kuu ya mashindano.


Kanuni za mashindano zinasema kwamba timu zenye nafasi za tatu za kwanza zinafikia raundi kuu ya Kombe la Dunia la mpira wa  Mikono.


Misri inakaribisha  Mashindano ya  Ulimwenguni  kwa mpira wa mikono mnamo 13 hadi 31 Januari kwa ushiriki wa timu 32 kutoka nchi tofauti za ulimwengu, na mashindano ya dunia hayo hufanyika katika ukumbi uliofunikwa Borg Al Arab, ukumbi uliofunikwa katika mji mkuu mpya wa kiutawala, ukumbi wa Dokta Hassan Mostafa mjini 6 Oktoba, na ukumbi uliofunikwa katika shirika la Uwanja wa Kimataifa wa Kairo.

Comments