Waziri wa Michezo ahudhuria mechi kati ya Qatar na Bahrain kwenye Mashindano ya Mikono Duniani kwenye ukumbi wa Uwanja wa Kairo

 Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, akiambatana na Dokta Hassan Mustafa, Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa mikono, na Mhandisi Hisham Nasr, Rais wa Shirikisho la Mpira wa mikono la Misri, walishuhudia mechi kati ya timu za Qatar na Bahraini katika duru kuu ya Mashindano ya dunia ya Mpira wa mikono , yanayokaribishwa kwa  Misri mnamo kipindi cha 13 hadi 31 Januari kwa ushiriki wa nchi 32 tofauti za ulimwengu.


Hiyo inakuja ndani ya mfumo wa shime ya Waziri wa Vijana na Michezo kuhudhuria mechi za mashindano na kufuata taratibu za udhibiti na kinga za mashindano zinazohusiana na virusi vya Corona

 zinazoteklezwa kwa wajumbe na timu zinazoshiriki mashindano hayo.


Comments