Al-Anani: Uzinduzi wa "Mobile Application" kuboresha Utalii


 Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale ilitangaza kuzindua Fomu ya simu ya "Mobile Application" ili kukuza Utalii wa Misri.


 Dokta Khaled Al-Anani, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, alifanya mkutano katika makao makuu ya Wizara huko Zamalek pamoja na wajumbe wa Kamati za kueneza, Maonesho ya nje, na shughuli za ndani , kujadili njia za mpango wa kufufua mambo ya ndani na harakati za nje za utalii na kutia juhudi ya kuonesha vituo tofauti vya kipekee vya kiutalii na kiakiolojia nchini Misri.


 Wakati wa mkutano, imejadiliwa kufufua harakati za Utalii za ndani kupitia kuandaa safari kwa wanafunzi wa shule na vijana wa vyuo vikuu kwa mikoa tofauti ya kiutalii, pamoja na kuanzisha shughuli za kiutalii na kiakiolojia,  mipango kadhaa ya kuongeza uwiano na uhamasishaji kwa Utalii na  akiolojia kati ya matabaka yote ya jamii , ikiwa ni pamoja na vijana na wazee, wanafunzi wa shule na vyuo vikuu na wale walemavu.


Comments