El-Sisi awapongeza Al-Ahly kwa shaba ya Kombe la Dunia


Rais Abd El Fatah El-Sisi aliipongeza Klabu ya Al-Ahly kwa kuishinda  medali ya shaba katika Kombe la Dunia kwa klabu.

Pongezi zangu za dhati kwa timu ya mpira wa miguu ya Al-Ahly kwa kushinda nafasi ya tatu kwenye Kombe la Dunia kwa Klabu na kwa kazi yao bora.

Kwenye ukurasa wake binafsi wa Tovuti za kijamii, Rais ameshachapisha "Pongezi zangu za dhati kwa timu ya mpira wa miguu ya Al-Ahly kwa kushinda nafasi ya tatu kwenye Kombe la Dunia la Klabu na kwa utendaji wao mzuri".

Aliendelea, "Nasisitiza  kuwa serikali haitaacha kusaidia na kudhamini michezo na vijana wa Misri katika michezo yote ya pamoja na ya mtu binafsi, akitamani maendeleo zaidi na zaidi kwa michezo ya Misri katika ngazi zote za kikanda na kimataifa.

Comments