Wizara ya Vijana yaendelea kutekeleza shughuli za mradi wa "Wasichana elfu moja..Ndoto elfu moja"

Katika mwendelezo wa Ushirikiano kati ya Baraza la utamaduni la Uingereza na Wizara ya Vijana na Michezo,Wizara huendelea kitekeleza shughuli za mradi wa  "Wasichana Elfu Moja..Ndoto elfu moja" kwenye mikoa tofauti  ya Jamuhuri.

Hiyo inakuja ndani ya mfumo wa jukumu la kijamii linalotolewa kwa Wizara ya Vijana na Michezo , kupitia kupanua msingi wa mazoezi ya michezo na umuhimu wa michezo kwa wanawake, kulingana na maagizo ya uongozi wa kisiasa.


 Shughuli za mradi zitaanza  kwenye  mikoa kadhaa : "Aswan, El Wadi El Gedid, Luxor, Sohag, Assiut, Minya, Beni Suef, Qena, Kairo, Qalyubia, Gharbia, Menoufia, Sharkia, Matrouh, Aleskandaria, Damietta, Port Said, Ismailia, Beheira. ”Na utekelezaji wa mradi huo unasimamiwa kwa idara ya ufundi yenye wakufunzi wataalam walioidhinishwa na Shirikisho la Soka la Uingereza.


Katika suala hilo, Waziri wa Vijana na Michezo Dokta Ashraf Sobhy alisema kuwa mpango huo unakusudia kupitia ufuatiliaji wa kiufundi wa wakufunzi wa waalimu kutoka kwa Programu ya Ujuzi wa Ligi Kuu ya  Ungereza ili kutumia sheria za Maadili ya Kanuni za Baraza la Utamaduni la Uingereza na programu ya Ujuzi wa kimsingi , ambazo muhimu zaidi  ni Usalama na Amani zaa watoto kabla ya Wakati na baada ya shughuli za michezo kwa shughuli za programu mahali popote au jamii yoyote.


Sobhy ameshaongeza kuwa mpango huo pia unakusudia kutekeleza sheria hizo na kulinda watoto wanaoshiriki, bila kujali jinsia, aina , rangi, imani, au ulemavu, na kuwalinda kutoka kwa aina anuwai za unyanyasaji, iwe ni ya mwili, ya kingono au ya kisaikolojia ambayo watoto hufunuliwa wakati wa mazoezi ya shughuli za michezo chini ya mwavuli wa programu.


Inaashiriwa kuwa mradi huo unatekelezwa kwa kushirikiana pamoja na Baraza la Utamaduni la Uingereza la kufanya mikutano ya michezo kwa wasichana kwenye Khomasi ya mpira wa miguu.Vituo 51 pia vimeanzishwa na makocha kadhaa ambao wamepata kozi ya ujuzi wa kwanza "primer skills  wameshahitimu .

Comments