Waziri wa Michezo aongoza mbio za matembezi katika Jiji la Michezo huko Mji Mkuu wa Utawala


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, aliongoza mamia ya vijana katika mbio za matembezi ya miguu, kabla ya ufunguzi wa shughuli za tamasha kuu la Shirikisho la Vituo vya Vijana wa Misri chini ya kauli mbiu "Vijana wa Misri kwenye ardhi ya mafanikio ".


Tamasha hilo limeandaliwa kwa Shirikisho kuu la Vituo vya Vijana wa Misri kwa kushirikiana na Utawala wa Kati wa Vituo vya Vijana na Mamlaka katika Wizara ya Vijana na Michezo, Shirikisho la Skauti na Miongozo la kimisri, Shirikisho la Misri la Michezo ya Elektroniki, na Mfuko wa Udhibiti na Matibabu ya uraibu na kuchukua dawa za kulevya.


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, anashuhudia shughuli za tamasha, pamoja na ushiriki wa vijana wa kiume na wa kike wa vituo vya vijana katika mikoa tofauti ya Jamuhuri na Jopo la wandishi wa vyombo vya Habari .

Comments