Waziri wa Michezo ashuhudia uzinduzi wa Mashindano ya mpira wa wavu ya kiafrika kwa Vijana wenye miaka U-21


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alishuhudia hafla ya ufunguzi wa Mashindano ya mpira wa wavu ya Afrika kwa Vijana wa U-21, yanayokaribishwa kwa Kairo mnamo kipindi cha Februari 20 hadi Februari 25 .


Sherehe ya ufunguzi ilijumuisha vikundi vya muziki na ushiriki wa Bendi ya Wizara ya Vijana na Michezo.


Waziri wa Michezo pamoja na mwenzake wa Congo wamefuatilia mechi ya timu ya Vijana wa Mpira wa wavu, katika mfumo wa mechi ya ufunguzi wa Michuano,na hivyo kwa mahudhurio ya Adnan Al-Bakbak, Makamu wa Rais wa shirikisho la Afrika na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Maandalizi ya Shirikisho la Afrika, Sameh Hamdy, Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Maandalizi ya Mashindano, Dokta Ahmed Al-Sheikh, Mkurugenzi Mtendaji wa Wizara ya vijana na michezo, na Jopo la wahusika.


Waziri wa Michezo  wakati akitoa beji ya kuanza kwa mashindano ameshasema"Tumefurahi na kuheshimiwa kuwakaribisha ndugu zetu waafrika nchini  Misri, ambayo imekuwa jukwaa la kufanya mashindano ya michezo ya kimataifa na mabara, tukitakia kila mtu kukaa vizuri katika nchi yao ya pili, Misri.


Waziri huyo ameshasema kuwa Mashindano ya mpira wa wavu ya Afrika kwa vijana  iliyokaribishwa kwa Misri kwenye ukumbi uliofunikwa wa Uwanja wa Kairo iko chini ya hatua kali za tahadhari kwa sababu ya kuenea kwa virusi vya Corona, ambayo ilikamilishwa vyema wakati wa Mashindano ya Mpira wa mikono ya Ulimwengu ulioandaliwa kwa Misri Januari iliyopita .


kuhusiana na hatua za tahadhari na kinga zinazotumika kwenye mashindano hayo, Sameh Hamdy, Mwenyekiti wa Shirikisho la mpira wa wavu na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Maandalizi ya mashindano , alielezea : baada ya kufikia Uwanja wa ndege wa Kairo, timu za taifa hizo zilifanya uchunguzi wa kitabibu kabla ya kuingia, wakati timu ya taifa ya Misri na wafanyikazi wote wa mashindano wakiwemo makocha, marefa, wasimamizi na wafanyikazi katika uwanja wa mashindano walifanya uchambuzi katika makao makuu ya Shirikisho, na mtu yeyote ambaye hakufanya uchambuzi hautaruhusiwa kuingia kwenye mashindano kabla ya kuanza kwa shughuli za mashindano.

Comments