Waziri wa Vijana na Michezo akutana na Mkurugenzi wa Maendeleo Endelevu wa kampuni ya Italia (ENI)


Jumanne, Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alikutana na Bwana Leonilovani, Mkurugenzi wa Maendeleo Endelevu katika kampuni ya Italia ENI, kuratibu kazi mnamo kipindi kijacho huko Kituo cha Vijana cha Sheikh Zaied katika mtaa wa kiemirati huko Mkoa wa Port said, kwa upande wa mafunzo ya wafanyikazi na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi juu ya mifumo ya kisasa ya usimamizi.


Waziri huyo alisisitiza kuwa maoni na mkakati wa Wizara hiyo zinategemea kukuza vituo vya vijana na kuinua ufanisi wao kwenye  Jamhuri yote, na kuwapa uwezo  unaoviwezesha kutekeleza jukumu lao katika kuwahudumia wachipukizi na vijana, pamoja na jamii inayozunguka ndani ya mfumo wa kuibadilisha kuwa vituo vya huduma za jamii.


Sobhy alisema kuwa Kituo cha Vijana cha Sheikh Zaied katika mtaa wa kiemirati kinawakilisha nyongeza mpya kwa vifaa vya vijana na michezo vilivyotawanyika  mkoani mwa Port Said, na tofauti ya majengo yake mbalimbali , na utayari wake wa kutoa kijamii, kiutamaduni, sanaa na michezo yote  kwa kuhudumia watu wa mtaa, akiashiria jukumu la kijamii la taasisi za kiuchumi na taasisi za sekta binafsi katika kutoa huduma za maendeleo Katika nyanja mbali mbali.


Ndani ya Kituo cha Vijana cha Sheikh Zared  katika makazi ya mtaa wa kiemirati katika mkoa wa Port Said ,kwa udhamini kutoka kampuni ya kiItalia Eni, hukuwepo mwendeshaji mkuu wa handaki ya Zohr ya uchimbaji wa gesi huko magharibi ya mkoa wa Port Said juu ya eneo la mita za mraba 4,747.


Kituo cha Vijana cha Sheikh Zared huko Port Said kinajumuisha jengo la kiutawala, maktaba, ukumbi wa kompyuta, ukumbi wa karamu, bustani ya watoto, viwanja viwili vya michezo, moja ya mpira wa miguu na nyingine kwa malengo anuwai, ukumbi wa mazoezi, na kumbi za shughuli.


Mkutano huo ulihudhuriwa na wakilishi wa kampuni ya Italia ya Eni, Bwana Marco Rotundi, Bwana Mahmoud Abu Al-Yazid, na viongozi wa Wizara ya Vijana na Michezo.

Comments