Karate yajiandaa kushiriki mashindano ya Ligi Kuu huko Uturuki


Timu ya Kitaifa ya Karate ya Misri inajiandaa ili kucheza katika mashindano ya Ligi Kuu ya Kimataifa, inayoamuliwa kufanyika mnamo kipindi cha Machi 10 hadi 15 Machi, ambayo ni mashindano ya kwanza ya msimu ambao wachezaji wanatamani kukusanya alama ili kufikia  Michezo ya Olimpiki ya Tokyo msimu ujao wa joto.Orodha ya  wachezaji wanaoshiriki  inajumuisha 19; wachezaji wa Kumite 12 na wachezaji 7 wa Kata.


Wachezaji wa Kumite ni: Mohamed Salah Abdel Hamid mwenye uzito wa kilo 60, Ali Al-Sawy, na Abdel-Rahman Hatem uzito wa kilo 67, Abdullah Mamdouh uzito wa kilo 75, Muhammad Ramadan uzito wa kilo 84 , Taha Tariq mwenye uzito wa + kilo 84, Reem Ahmed Ramzi Kwa kilo 50, Yasmine Hamdy kwa kilo 55, Firrial Ashraf kwa uzito wa kilo 68, Shaima Abu Al-Yazid, Suhaila Ahmed, Habiba Majed kwa + kilo 68.


Wachezaji wa Kata ni: Sarah Asim, Aya Hisham huko Kata ya mmoja, Ziyad Muhammad Abd al-Rahman, Yusef Ashraf Ahmed, Ali Muhammad Abd al-Hay, Aya Hesham Muhammad, na Asma Majdi Abdullah, Taqi Hesham Farouk.


Timu hiyo inaongozwa na kocha Mohamed Abdel-Rahman (Mkufunzi wa wanaume wa Kumite), Hani Qeshta (Mkufunzi wa Kumite kwa wanawake), na Hani Mahmoud (Mkufunzi wa Kata), na ujumbe huo unasimamiwa na Dokta Saleh Atris.

Comments